Saturday, 11 January 2014
RWANDA YAKANUSHA UVUMI KUHUSU KIFO CHA KAGAME

Ikulu ya Rais wa Rwanda imekanusha uvumi ambao umekuwa unazidi kuenea kuhusu kifo cha Rais Paul Kagame, ambao umepelekea raia wa mji wa Goma kuandamana mabarabarani wakisheherekea kwa furaha taarifa hio.
WATOTO WAWILI WAFARIKI KWA KULIPUKIWA NA KITU KINACHOSADIKIWA KUWA NI BOMU JIJINI DAR...

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Temeke, Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP), Engelbert Kiondo.
Friday, 10 January 2014
HAYA NI MADHARA YANAYOWEZA KULETWA NA HENNA AMBAYO SI YA MMEA...

f you're thinking of getting a fake tattoo over Spring Break, you might want to think again.
According to the US Food and Drug Administration, while temporary body art may involve less commitment than permanent ink, it's certainly not harmless and could result in a trip to the emergency room.
MedWatch, the FDA's safety and health complaints hotline, has had scores of consumers report bad side effects to the fleeting markings, including redness, blisters, raised red weeping lesions, loss of pigmentation and even permanent scarring.
SABABU YA KIFO CHA MPENDWA WETU ZAINAB BUZOHERA
Zainab Buzohera enzi ya uhai wake
Siku ya Ijumaa Jan 3, 2014 baada ya kuanza kujisikia vibaya Marehemu
Zainab alikwenda Hospitali ya Doctor's Community iliyopo Lanham,
Maryland ambayo ni kama maili 7 kutokea nyumba kwake kwenye mji wa
Bladensburg, Maryland.aliokuwa akiishi enzi ya uhai wake. Siku hiyo
usiku wa saa 5 usiku marehemu alifika hospitali kitengo cha Emergency
baada ya kuanza kujisikia kushindwa kupumua na baada ya kuchekiwa na
madaktari walimkuta na tatizo la homa ya mapafu (Pneumonia stage 3).
Baada
ya madaktari kugundua tatizo la Zainab ni kubwa, Siku ya Jumamosi Jan
4, 2014 Mpendwa wetu alipatiwa kitanda kwenye wodi ya wagonjwa mahututi
(ICU) huku akiwekewa mashine ya Oxygen ili kumsaidia kupumua. Mpendwa
wetu alishawahi kulazwa hospitali siku za nyuma lakini kinachowashangaza
wengi hasa marafiki zake wa karibu ni jinsi alivyowapigia simu karibu
kila mmoja na kuwaeleza kulazwa kwake siku hiyo jambo lililotafsiliwa na
wengi wakiwemo marafiki zake kwamba alishajua mauti itamkuta na
kuwapigia simu huko ilikuwa anawaaga.
MKAPA AIPONDA MISAADA KUTOKA NJE, ASEMA YADHOOFISHA UCHUMI AFRIKA
Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Benjamin William Mkapa amesema misaada inayotolewa na nchi za Magharibi kwa nchi za Afrika haina masilahi na ina lengo la kudhoofisha ukuaji wa uchumi wa nchi za Afrika .
AMUUA BABA YAKE KUMUOKOA SHANGAZI YAKE ALIYEKUWA ANABAKWA- NACHINGWEA
Mkazi wa mmoja wa kijiji cha Nang’ondo, Wilaya ya Nachingwea, mkoani Lindi anashikiliwa na jeshi la polisi baada ya kumuua baba yake mzazi katika harakati ya kumwokoa shangazi yake aliye alikuwa anabakwa.
WAZIRI KIGODA : MFUMO MASHINE EFDs NI MBOVU, UNAKANDAMIZA ...
Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Abdallah Kigoda.
Serikali imekiri mfumo wa ulipaji kodi na ule wa utumiaji wa mashine za kutolea risiti(EFDs) kuwa ni mbovu na hivyo unahitaji kufanyiwa kazi.
IGP ATANGAZA MABADILIKO MAKUBWA JESHI LA POLISI.

Mkuu Mpya wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali, Ernest Mangu ameanza kazi kwa kutangaza mabadiliko ya mfumo wa jeshi hilo huku akiunda vitengo vipya kwa lengo kuongeza ufanisi katika kukabiliana na uhalifu.
Thursday, 9 January 2014
MADAWA YA KULEVYA YAINGIZWA SUPERMARKET KATIKA MAKASHA YA NDIZI

Polisi akiwa analinda makasha yenye dawa za kulevya yaliyoingizwa
nchini Ujerumani kutoka Columbia kwa kuwekwa ndani ya ndizi

Polisi akifungua moja ya nizi ambazo ndani yake kuliwekwa dawa za kulevya
Wizara ya maliasili na utalii imewasimamisha kazi watumishi wake 22 wa idara ya wanyama pori
Wizara ya maliasili na utalii imewasimamisha kazi watumishi wake
ishirini na mbili wa idara ya wanyama pori wanaotuhumiwa kushiriki
katika vitendo vya ujangili dhidi ya wanyama pori, hujuma, pamoja na
vitendo vya rushwa na hatua za kisheria zinaendelea kuchukuliwa dhidi
yao.
Magonjwa ya mlipuko yanukia jijini Dar
Pichani
ni magari ya kuzolea taka ngumu ya kampuni mbalimbali yakiwa kwenye
foleni ya kuingia Dampo la Pugu Kinyamwezi ambalo miundo mbinu yake ni
mibovu na kupelekea zoezi hilo kuchukua zaidi ya siku 4 mpaka
kufanikisha kufikia eneo maalum la kumwagia taka ngumu.
.Ni kutokana na kukwama kwa magari ya taka kwenye Dampo la Pugu
.Siku ya tatu sasa magari ya taka yamekwama
Serikali ya China imemtoza faini ya zaidi ya dola milioni moja mtengeza filamu mashuhuri nchini humo, Zhang Yimou kwa kwenda kinyume na sera ya mtoto mmoja kwa kila familia nchini humo.

Serikali ya China imemtoza faini ya zaidi ya dola milioni moja mtengeza filamu mashuhuri nchini humo, Zhang Yimou kwa kwenda kinyume na sera ya mtoto mmoja kwa kila familia nchini humo.
MAWAZIRI WAPYA WATANO WATAJWA TANZANIA
RAIS Jakaya Kikwete anatarajia kutangaza majina ya mawaziri watano mapema wiki hii,taarifa za ndani kutoka Ikulu ya Rais Kikwete iliyonaswa na Habarimpya.com zinaeleza kwamba, zoezi hilo limepangwa kufanyika mapema wiki hii kabla ya Rais kuanza zoezi la kuteuwa wabuge wa bunge la Katiba.
SUMAKU MAALUM YANASA WEZI WA NONDO JIJINI

SUMAKU maalumu zilizofungwa kwenye lango la kuingia kwenye mradi wa ujenzi wa daraja la Kigamboni, zimesaidia kukamata wezi wa nondo na misumari.
“Wizi upo, lakini tumekabiliana nao, ilibainika kuwapo watu wa nje wanaojichomeka kwenye kazi na kuiba, walikuwa wanajivisha vipande vya nondo maungoni na kujifunga, wengine kutumia nywele ndefu kuficha zaidi ya nusu kilo ya misumari. “Tulifunga sumaku maeneo ya kutokea na kuingia na baadhi walivutwa nayo kutokana na vyuma walivyoficha maungoni na kukamatwa kirahisi sana, sasa wizi umepungua,” amebainisha Meneja Mradi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Karim Mataka.
HUJAFA HUJAUMBIKA... MIAKA 29 KITANDANI MUHIMBILI NA HANA NDUGU..
ALIPOPANDA basi kutoka Tanga kuelekea Dar es Salaam mwezi fulani mwaka 1984, hakujua kama ilikuwa ni siku yake ya mwisho kuwa mzima, mwenye mwili mkakamavu uliokamilika viungo vyote.
Wednesday, 8 January 2014
BREAKING NEWS: FIFA YAHAMISHA MUDA WA KOMBE LA DUNIA MWAKA 2022 HUKO QATAR
Baada ya utafiti wa muda mrefu na majadiliano yaliyochukua zaidi ya mwaka mmoja shirikisho la soka ulimwenguni limefikia uamuzi wa kutofanyika kwa mashindano ya kombe la dunia kwa mwaka 2022 katika kipindi cha msimu wa kiangazi .
Kwa mujibu wa katibu mkuu wa FIFA Jerome Valcke michezo ya kombe la dunia haiwezi kufanyika kwa msimu huo nchini Qatar kutokana na hali ya hewa kuwa joto kali na hivyo kuhatarisha afya na usalama wa wachezaji.
HABARI ZA KIMATAIFA/ WAUMINI WAUAWA MSIKITINI NCHINI NIGERIA

Watu waliojihami wameshambulia msikiti katika jimbo la Kano Kaskazini mwa Nigeria na kuwaua waumini watatu huku wakiwajeruhi wengine 12. Polisi wanasema kuwa watu hao waliwafyatulia risasi waumini waliokuwa msikitini katika kijiji anakoishi gavana wa jimbo hilo, Rabiu Musa Kwankwaso.
BALOZI WA TANZANIA NCHINI MAREKANI LIBERATA MULAMULA AKUTANA NA VIONGOZI WA NSSF
Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Liberata Mulamula, akizungumza na uongozi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dar es Salaam, kuwataka NSSF kufungua Ofisi zitakazotoa huduma za Westadi nchini Marekani ambazo zitawasaidia watanzania waishio nje ya nchi kusafirisha mwili wa marehemu pamoja na kupata huduma ya matibabu kwa ndugu wanne waliopo nchini. Kushoto ni Kaimu Meneja Kiongozi na Huduma kwa Wateja wa NSSF, Theopista Muheta.
KITU KIPYA TOKA KWA JAGUAR.".KIOO" VIDEO ALIYOSHOOT NA WAFUNGWA GEREZANI NCHINI KENYA...
Kioo ni wimbo ambao unaelezea safari ya maisha yake jinsi ambavyo hujitazama kila wakati kwenye kioo kuona jinsi alivyopiga hatua ndefu.
LULU AMPONGEZA MAMA KANUMBA KWA SIKU YAKE YA KUZALIWA...AANDIKA UJUMBE MURUA!

Mama Kanumba atakuwa ametimiza miaka kadhaa hivi sasa na amepokea zawadi ya keki kutoka kwa muigizaji Elizabeth Michael.
KUFUATIA MWANAMKE KUKAMATWA NA DAWA ZA KULEVYA, DR. MWAKYEMBE ATEMBELEA UWANJA WA NDEGE DAR ES SALAAM
![]() |
| Mhe. Mwakyembe. |
KITENGO Cha Usalama wa Taifa
Nchini kinatarajia kuogeza nguvu katika kuimarisha ulinzi katika viwanja vya ndege nchini ili
kukabiliana na wimbi kubwa la usafifirishaji wa dawa za kulevya pamoja na
madini hapa nchini hususani katika kiwanja cha ndege cha kimataifa
Mwalimu Julius Nyerere (JNA) kilichopo jijini Dar es Salaam.
TANZANIA HAITISHWI MAJIRANI KUJITENGA.....NI KUTOKANA NA HATUA YA RWANDA UGANDA NA KENYA KUTUMIA KITAMBULISHO KAMA PASI ZA KUSAFIRIA
Ni kutokana na hatua ya Rwanda, Uganda na Kenya kutumia vitambulisho kama pasi za kusafiria
Serikali imesema kuwa hatua iliyoanzishwa na nchi za Rwanda, Kenya na Uganda ambayo imeruhusu raia wake kusafari ndani ya nchi hizo kwa kutumia vitambulisho vya taifa badala ya hati ya kusafiria kuwa siyo tishio.
Subscribe to:
Comments (Atom)




































