Zainab Buzohera enzi ya uhai wake
Siku ya Ijumaa Jan 3, 2014 baada ya kuanza kujisikia vibaya Marehemu
Zainab alikwenda Hospitali ya Doctor's Community iliyopo Lanham,
Maryland ambayo ni kama maili 7 kutokea nyumba kwake kwenye mji wa
Bladensburg, Maryland.aliokuwa akiishi enzi ya uhai wake. Siku hiyo
usiku wa saa 5 usiku marehemu alifika hospitali kitengo cha Emergency
baada ya kuanza kujisikia kushindwa kupumua na baada ya kuchekiwa na
madaktari walimkuta na tatizo la homa ya mapafu (Pneumonia stage 3).
Baada
ya madaktari kugundua tatizo la Zainab ni kubwa, Siku ya Jumamosi Jan
4, 2014 Mpendwa wetu alipatiwa kitanda kwenye wodi ya wagonjwa mahututi
(ICU) huku akiwekewa mashine ya Oxygen ili kumsaidia kupumua. Mpendwa
wetu alishawahi kulazwa hospitali siku za nyuma lakini kinachowashangaza
wengi hasa marafiki zake wa karibu ni jinsi alivyowapigia simu karibu
kila mmoja na kuwaeleza kulazwa kwake siku hiyo jambo lililotafsiliwa na
wengi wakiwemo marafiki zake kwamba alishajua mauti itamkuta na
kuwapigia simu huko ilikuwa anawaaga.
Mmoja
wa marafiki zake anayeishi Maryland alielezea siku ya harambe kwamba
Zainab ameishaugua kabla ya hapo laikini hajawahi kumpigia simu, hii
ilikua ni mara ya kwanza na alipokwenda hospitali anakumbuka maneno
aliyoambiwa na marehemu kwamba " hewa hiyo itumie wakati unanafasi
angalia mimi pamoja na hewa yote hiyo kuwepo nimewekewa Oygen"
Baadae
madaktari walimkataza asiongee na simu kwani anahitaji kupumzika badala
yake Zainab alianza kuwatext marafiki zake kuwaelezea jinsi
anavyoendelea. Japokuwa baadae kutexti nako alikatazwa na text ya mwisho
alimtextia Dullah akimwambia amekatazwa asitext tena. Ndipo ilipofika
saa 2 usiku siku hiyo ya Jumamosi Jan 4, 2014 mpendwa wetu aliaga Dunia.
Dullah
na Zainab wapo wako pamoja si chini ya miaka 17, tangia Ukonga Banana
walipokuwa wakiishi jirani wakiwemo Saidi Mwamende na dada yake Nuru na
Mpendwa wetu Zainab ndiye aliyetangulia kuja Marekani mwaka 2000 na
mwaka uliofuatia Dullah akaungana naye.
Mpendwa wetu
Zainab na Dullah walishaoana Kiserikali na walikuwa na mipango ya kwenda
wote nyumbani kati ya mwezi march au April kwenda kutia ubani ndoa yao.
Zainab sisi tulikupenda lakini Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema
amekupenda zaidi, daima utakumbukwa, mama, baba, kaka, dada, wadogo
zako, ndugu, jamaa na marafiki bila kumsahau kipenzi chako cha rohoni
Dullah.
Inna lillahi wainna ilayhi rajiuun
Dullah na Zainab Enzi hizo za Ukonga Banana
Mwili
wa mpendwa wetu uliondoka siku ya Alhamisi Jan 9, 2014 badala ya
Jumatano na unatarajiwa kufika Dar es Salaam, Tanzania siku ya Jumamosi
Jan 11, 2014 na maziko yatakuwa Jumapili siku inayofuata. Wasindikizaji
wao waishafika tangia Alhamisi.
CREDT VIJIMAMBO..
No comments:
Post a Comment