Saturday 11 January 2014
RWANDA YAKANUSHA UVUMI KUHUSU KIFO CHA KAGAME
Ikulu ya Rais wa Rwanda imekanusha uvumi ambao umekuwa unazidi kuenea kuhusu kifo cha Rais Paul Kagame, ambao umepelekea raia wa mji wa Goma kuandamana mabarabarani wakisheherekea kwa furaha taarifa hio.
Rwanda imeelezea mshangao wake kuona uvumi huo ukizagaa, huku raia wa mashariki ya Congo wakiandamana wakionyesha furaha kuhusiana na na taarifa isiyokua ya kweli.
Paul Kagame, mwenye umri wa miaka 56, ni rais wa Rwanda tangu mwaka wa 1994, baada tu ya waasi wa RPF kushinda jeshi la Rwanda lilokua likimuunga mkono rais Juvenal Habyarimana. Chanzo cha kushindwa kwa jeshi la Rwanda ni mauaji ya kimbari, ambayo lilihusishwa jeshi hilo.
CREDIT DAR 24
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment