Thursday, 9 January 2014

MADAWA YA KULEVYA YAINGIZWA SUPERMARKET KATIKA MAKASHA YA NDIZI

Polisi akiwa analinda makasha yenye dawa za kulevya yaliyoingizwa
 nchini Ujerumani kutoka Columbia kwa kuwekwa ndani ya ndizi
Polisi akifungua moja ya nizi ambazo ndani yake kuliwekwa dawa za kulevya


Mjini Berlin huko Ujerumani kwenye Supermarket zipatazo tano yamepatikana makasha yaliyojaa ndizi ambamo ndani yake kulikuwa na dawa za kulevya zilizofichwa zinazokadiriwa kuwa na uzito wa kilo mia moja arobaini.

Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa huu ni mtindo ambao umekuwa unatumiwa na wasafirishaji wa madawa ya kulevya. Hata hivyo safari hii kulifanyika makosa ya mawasiliano ambapo mpokeani alianza kuyasambaza makasha hayo kwenye Super Markets akidhaniwa kuwa ni ndizi.

Makasha ya kwanza yalifikishwa kwa muuza matunda kwa jumla kwenye mji hamburg baada ya kuwasili kwa meli kutokea Colombia ikiaminika kuwa ni ndizi.

Wafanyakazi wa hizi Supermarket ndio walitambua kuwa makasha ambayo ndani yake ndio kulikuwa na hizo kilo 140 za unga aina ya Cocaine saa kadhaa baada ya ndizi kuanza kuuzwa kwenye maduka yao.

CREDIT ..DAR 24

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!