Friday, 10 January 2014

MKAPA AIPONDA MISAADA KUTOKA NJE, ASEMA YADHOOFISHA UCHUMI AFRIKA

  Click image for larger version. 

Name: mkapa.jpg 
Views: 0 
Size: 19.7 KB 
ID: 131319

Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Benjamin William Mkapa amesema misaada inayotolewa na nchi za Magharibi kwa nchi za Afrika haina masilahi na ina lengo la kudhoofisha ukuaji wa uchumi wa nchi za Afrika .



Alisema kuwa mara nyingi nchi za Magharibi zimekuwa zikitoa misaada kwa masharti ya kutolewa kwa ushuru kwa bidhaa zinazoingia pamoja na bidhaa zinazouzwa katika mataifa hayo, jambo ambalo linaweza kudhoofisha ukuaji wa uchumi kwa nchi za Afrika .
Kauli hiyo aliitoa wakati akifungua Chuo cha Ualimu cha Benjamin Mkapa kilichopo Mchangamdogo Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba ikiwa ni katika shamra shamra za kutimiza miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar .
Alisema masharti hayo yanapaswa kuepukwa na viongozi wa nchi za Afrika na kusisitiza kwamba hayo yanaweza kuepukika ikiwa mataifa hayo yatawekeza zaidi katika sekta ya elimu kwa kuhakikisha wanawaandaa vijana kwa kuwapatia elimu bora .
“Misaada hii ina lengo la kudhoofisha ukuaji wa uchumi kwa mataifa ya Afrika, hivyo ni vyema viongozi wa mataifa hayo kuwa makini na masharti yanayotolewa , unafikiri unapoambiwa bidhaa zinazoingia nchini mwako zisitozwe ushuru Serikali itapata wapi mapato ? ” alihoji .
Akizungumiza miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar , alisema kuwa yameleta faida nyingi kwa Wazanzibari hasa katika sekta ya elimu ambapo yameondoa ubaguzi katika upatikanaji wa huduma muhimu za kijamii ikiwamo elimu, afya na mawasiliano.
Alibainisha kwamba kufanyika kwa Mapinduzi hapo Januari 1964 kuliondoa aina zote za udhalimu wa kikoloni ambao uliwafanya wenyeji wa visiwa hivi kuwa nyuma kutokana na kukosa fursa ya
“Ni lazima tukiri kwamba Mapinduzi ya Januari 12, 1964 ndiyo yaliyowaweka wananchi wa Zanzibar katika hali ya umoja , kupendana na kusaidiana kwani yaliondoa minyororo ambayo ilikuwa inakwaza kufikia maendeleo ”alieleza Mkapa.

JAMII FORUM...

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!