Saturday 29 June 2013

JAMANI KWA WALE WALIOKUWA HAWAJAMSIKIA MKENYA MWENYE HASIRA NA OBAMA JUU YA UJIO WAKE TANZANIA CHECK HAPO MKENYA ANAVYOMFUNGUKIA OBAMA


OBAMA ATOA SABABU ZILIZOMFANYA ASIENDE KENYA KWA SASA... SABABU KUBWA NI KESI YA UHURU KENYATTA NA MAKAMU WAKE



US President Barack Obama said Saturday the “timing was not right” for him to travel to Kenya, his father’s homeland, during his current Africa tour, but he expected to go there many times in the future.

Obama said the new government of President Uhuru Kenyatta was still finding its feet after an election in March, and that Nairobi was “still working out issues with the international community”.

He was referring to a looming trial for Kenyatta and Vice President William Ruto at the International Criminal Court for their alleged roles in deadly violence that killed more than 1,000 people after 2007 polls.

“The timing was not right for me as president of the United States to be visiting Kenya when those issues need to be worked on,” Obama said.

But the US leader said he had visited Kenya multiple times before he was president and expected to return.

“My personal ties to the people of Kenya, by definition are going to be strong and will stay strong,” he said.

Obama’s Africa tour started in Senegal, and he is currently in South Africa. He will wrap up his week-long journey in Tanzania.

Source: Capital fm

LULU BEFORE AND EFTER

HABARI ZA UMBEYA! JOKATE(KIDOTI) AIBUA KITU KIPYA NA KUKIANIKA WAZI MTANDAONI...

MWANAMITINDO daraja la kwanza Bongo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ amemwanika mwanaume mpya mtandaoni huku wakiwa wamepozi katika staili ya wapendanao.

Awali, paparazi wetu alitonywa na sosi aliyeomba hifadhi ya jina lake kuwa amemuona mwanaume mpya wa Jokate katika mtandao wa Instagram.

“Nimemuona Jokate na mwanaume wake mpya lakini simjui kwa jina, kama huamini ingia kwenye mtandao wa Instagram uone mtoto wa kike alivyojiachia katika pozi za kimahaba,” alisema sosi huyo.

Baada ya kuzinyaka habari hizo, paparazi wetu aliingia kwenye kilongalonga chake na kuperuzi katika mtandao huo kisha kujionea picha hizo, haraka sana akazisevu katika simu yake.

Aidha, wadau mbalimbali waliopo katika mtandao huo walitoa maoni mbalimbali huku wengi wao wakimpongeza

OBAMA WELCOME TANZANIA! ........ KITU KIPYA TOKA KWA TIMAMU EFFECT KWA AJILI YA UJIO WA OBAMA NCHINI TANZANIA.



UFUNGUZI WA MKUTANO WA SMART PARTNERSHIP DIALOGUE 2013.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na viongozi mbalimbali pamoja na vijana wa umri wa CPTM 29ers waliohudhuria mkutano wa Smart Partneship Dialogue 2013 wakati wa ufunguzi rasmi wa mkuatno huo unaoshirikisha watu zaidi ya 800 katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere Convention Centre jijini Dar es salaam Ijumaa Juni 28, 2013
 
 


Viongozi mbalimbali wa nchi za Afrika wakishiriki katika mijadala na vijana wa CPTM 29ers 
Mjadala ukiendelea
 




Meza kuu wakifurahia onesho la THT.
 
Rais Kikwete akipiga ngoma kuashiria mwisho wa mjadala wa viongozi na vijana




Sehemu ya wageni
Wanahabari wa ndani na nje ya nchi wakirekodi tukio hilo la kihistoria
 

VUNJA MBAVU!




HICHO NDICHO KISA CHA KASEJA KUACHWA NA SIMBA

Photo: Juma Kaseja ONDOKA SIMBA...!!!!1
 
 
 
Japokuwa haija wekwa wazi sababu rasmi ya kuachwa kwa kipa Juma Kaseja, imebainika kwamba ni kipigo cha mabao 2-1 dhidi ya mahasimu wao Yanga.
Simba ilipokea kipigo hicho, katika mchezo wa funga dimba wa Ligi Kuu Bara uliopigwa Mei 18 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambapo Kaseja Ndiye aliyekaa langoni.
 

Habari za kuaminika toka ndani ya uongozi wa Simba zinaeleza kuwa kipigo hicho kiliwakera viongozi wa klabu hiyo kukiwa na madai kuwa kilitokana na uzembe au makusudi.

Kiongozi mmoja wa Simba ameuambia Mtandao huu kuu pamoja na upungufu mwengine ambao kipa huyo amekuwa akihusishwa nao, mazingira ya mabao mawili dhidi ya Yanga, ndiyo yamemwondoa Msimbazi.

“Kaseja ni kipa mzuri, hivi unavyomfahamu anaweza kufungwa mabao kama yale? Kwa kweli hilo limetuacha na maswali mengi kichwani, imetukera sana, mwache aende zake akatafute maisha sehemu nyingine,” alisema kiongozi huyo kwa sharti la kutotajwa jina.

Akienda mbali zaidi, kiongozi huyo alisema ingekuwa vizuri zaidi kama Kaseja angeweza kuonesha umahiri wake na kuondoa dhana mbovu dhidi yake, lakini kitendo cha kukubali nyavu zake kutikiswa kilitoa jawabu juu ya maswali waliyokuwa nayo.

Siku za karibuni kumekuwa na utata juu ya Kaseja kubaki Msimbazi baada ya mkataba wake kufikia mwisho huku akizua mgawanyiko miongoni mwa wajumbe wa Kamati ya Usajili kwa wengine kutaka asajiliwe na wengine wakitaka aachwe.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa klabu hiyo Alhaj Ismail Aden Rage, Kaimu Makamu Joseph Itang’are ‘Kinesi’ na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Zakaria Hanspoppe, kwa nyakati tofauti walisema Kaseja hawezi kuongezewa mkataba.

Viongozi hao walitoa kauli hizo bila ya kueleza wazi sababu za kumuacha kipa huyo namba moja wa timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ ambaye ameitumikia klabu hiyo karibu miaka 10.

Hayo yakiendelea, Kaseja mwenyewe  hakuwa tayari kusema lolote, ingawa kuna habari kuwa huenda akatua Coastal Union ya Tanga au Mtibwa Sugar ya Turiani.

Aidha, Yanga imemnasa mshambuliaji wa Mtibwa Sugar, Husssein Javu ambaye pia alikuwa akiwaniwa na Simba.

Habari kutoka Yanga, zinasema nyota huyo amesaini mkataba wa miaka miwili kwa ajili ya kuitumikia klabu hiyo.

AKINA KAKA HAWA NI WANAMITINDO MAARUFU NCHINI MAREKANI. HAYA SASA!

NSSF MKOA WA NJOMBE WATOA MISAADA KITUO CHA WATOTO YATIMA UWEMBA.

 

 Hapa ndiko kituo cha Watoto yatima cha Uwemba kilipo na haya ni Majengo ya Misheni ya Uwemba Njombe.

 Sister Agape Mgaya ambaye ni mlezi wa Kituo cha Watoto yatima cha Misheni Uwemba  akitoa maelekezo kwa Msafara wa NSSF Mkoa wa Njombe uliofika kutoa misaada mbalimbali kwa
watoto yatima leo.


 Meneja wa NSSF Mkoa wa Njombe bwan Godwin Mwakalukwa akiwatizama watoto yatima Kituoni hapo leo

 Baadhi ya Vitu vikikabidhiwa na Meneja wa

Friday 28 June 2013

NILIKUWA SIJAWAHI KUSIKILIZA HUU WIMBO KWA MAKINI UNA UJUMBE SAFIII.AISEE!.........WEEKEND NJEMA WADAU WA SOPHIE MBEYU BLOG NAWAPENDAJEE SASA

 

DRESS OF THE DAY,(COCKTAIL DRESS) HII NI NGUO SPESHO KWA KUTOKEA HASWA JIONI

RAIS KIKWETE AFANYA UKAGUZI WA MWISHO WA MAANDALIZI YA SMART PARTNERSHIP UNAOFUNGULIWA LEO JIJINI


Wadau wa IT kutoka E ducation wakisalimiana na Rais Kikwete

Rais Kikwete akiwa katika banda la Malaysia

Rais Kikwete  akiwakatika Banda la HAUWEI akiangalia teknologi ya kisasa yaTELEPRESENCE ambayo imeshaanza kutumika nchini.

MAJANGAZ! SAADAH ALLY KILONGO AKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA YENYE THAMANI YA MILIONI 170!!!!



pretty saadah


Siku ya graduu yake mwaka jana apooo


A BUSINESSWOMAN, Saada Kilongo (26), appeared before the Kisutu Resident Magistrate's Court in Dar es Salaam yesterday charged with trafficking narcotic drugs worth more than 170m/-.

Before Senior Resident Magistrate Nyigulila Mwasebo, the accused was not allowed to enter any plea to the charge. She was remanded until July 10, this year, when the case will be mentioned.

State Attorney Peter Maugo alleged that on June 24, this year, the accused, a resident of Mbezi beach Rainbow was found trafficking narcotic substances namely ephedrine HCL at Julius Nyerere International Airport (JNIA). The prosecutor said that the drugs were valued 170,481,000/ 

Haya sasa hii ndio habari ya mujini kah!! mwenyez mungu atuepushe na tamaa na mabalaa kama haya, so sad jaman na amemaliza chuo last year, im speechless!!!
UMJINI KAZI!!
 
 
 
 
 
SOURCE. ZEDDYLICIOUS.

MWANAMITINDO LINDA BEZUIDENHOUT AWASHUKURU FANS WAKE.


RAIA WA AFRIKA KUSINI WAKESHA KUMUOMBEA NELSON MANDELA.

Raia wa Afrika kusini wamekesha kwa maombi maombi nje ya makaazi ya zamani ya aliyekuwa rais wa taifa hilo Nelson mtaani Soweto.
Rais Jacob Zuma amesema kuwa afya ya shujaa huyo aliyepigana dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini humo inaendelea kuimarika.
Mandela aliye na umri wa miaka 94 amekuwa hospitalini akiuguwa ugonjwa wa maambukizi ya mapafu.

AZIKWA AKIWA HAI.


Kazi ya ufuakuaji lili kutoa mwili wa mzee huyo ambaye alifukiwa akiwa hai, ikiendelea.


MWILI WA ALIEZIKWA AKIWA HAI BAADA YA KUTOLEWA KABURINI
MDOGO WA MAREHEMU ALIEZIKWA AKIWA HAI

WANANCHI HAO HAIKUTOSHA BAADA YA KUMZIKA MWENZAO AKIWA HAI WALIKWENDA KUCHOMA NYUMBA YAKE







KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida wananchi wa kijiji na kata ya Mkwajuni Wilaya ya Chunya Mkoani hapa wamemzika Mwanakijiji mwenzao akiwa hai wakimtuhumu kusababisha kifo cha Mkazi mmoja kijijini hapo.
  
Tukio hilo la kusikitisha limetokea Apri 26 mwaka huu  majira ya Saa Nane Mchana katika Kitongoji cha Maweni Makaburini baada ya Mhanga aliyefahamika kwa jina la Victory Mwachirui(68) kuhudhuria mazishi ya Pita Barton(28)aliyefariki baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, Thobias Ismail amesema marehemu alipatwa na umauti akiwa anapatiwa matibabu kwa mganga wa jadi ambaye jina lake halikuweza kujulikana maramoja.

Amesema wakati taratibu za mazishi zikiendelea Ndugu wa marehemu walidai kuwa kifo cha Marehemu kilisababishwa na Mwachirui ambaye ni Katekista mstaafu kwa imani za kishirikina.

Ameongeza kuwa wakati kaburi likichimbwa kwa ajili ya kumzika  marehemu ndipo vijana waliokuwa wakichimba waliagiza Wazee wa Mila wafike makaburini kwa ajili ya kuangalia utaratibu wa mazishi na kukagua ukubwa wa Kaburi ambalo lilikuwa limekwisha chimbwa.
  
Kutokana na mwito huo walifika wazee wanne akiwemo Mzee Mwachirui ambaye walimsisitiza kusogea jirani na kaburi ambapo baada ya kusogea alipigwa na Sururu kichwani na kuangukia kaburini huku akisindikizwa na marungu.
  
Baada ya Mzee huyo  kupoteza fahamu Vijana hao walianza kutandika fito ndani ya kaburi kisha kufukia kwa udongo kiasi kwa lengo la kutenganisha na Mwili wa Marehemu Pita uliokuwa kwenye jeneza baada ya kuwazika kwenye kaburi moja.
  
Baada ya kukamilika kwa zoezi la mazishi kundi la vijana lilielekea hadi nyumbani kwa Mzee aliyezikwa akiwa hai na kuiteketeza nyumba yake huku wakiapa kutotoa siri wakidai Siri ya Jeshi.
  
  
Jeshi la Polisi baada ya kufanya upelelezi na kubaini kitendo hicho waliwaamuru baadhi ya Vijana kufukua kaburi hilo zoezi ambalo lilifanyika baada ya Vijana hao kulipwa.
  
Baada ya kufukuliwa kwa kaburi hilo Mwili wa Marehemu Mzee Mwachirui ulichukuliwa na kupelekwa katika Hospitali ya Misheni ya Mkwajuni kwa ajili ya Uchunguzi huku Mwili wa Pita ukizikwa upya palepale.
  
Baada ya kukamilika kwa uchunguzi mwili wa marehemu ulikabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya mazishi ambapo Marehemu alizikwa katika eneo tofauti na alipokuwa amefukiwa awali.
  
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo pia ametoa wito na kuwaasa  wananchi na jamii kuacha tabia  ya kuamini mambo ya ushirikina na uchawi kwa madai kuwa hauna faida kwao bali huchochea migogoro katika jamii zao.

Aidha ameongeza kuwa wakumbuke kitendo cha kujichukulia sheria mkononi ni kosa kisheria ambapo pia  amewaomba wenye taarifa za walipo waliohusika na mauaji hayo kuzifikisha polisi haraka ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao ingawa hakuna aliyekamatwa kuhusika na tukio hilo.

Picha na E. Kamanga wa Mbeya yetu
 

BINTI AJIFUNGUA BARABARANI HUKO NJE KIDOGO YA MOROGORO.

Na Dustan Shekidele, Morogoro

BINTI mmoja aitwaye Josephine Michael mkazi wa Kijiji cha Kiegea nje kidogo ya Manispaa ya Morogoro, Jumatano iliyopita alijifungua barabarani wakati akikimbizwa hospitalini kwa kutumia usafiri wa bodaboda.
Josephine Michael akiwa barabarani baada ya kujifungua.
Tukio hilo lililowashtua watu wengi lilitokea asubuhi kwenye Kituo cha Daladala Cha Nanenane kandokando ya Barabara Kuu iendayo Dar es Salaam.

 Askari wa Barabarani alilazimika kuacha shughuli yake ya kuongoza magari na kusimamisha magari
kumsaidia Binti huyo ambaye alijifungua mtoto wa kiume.


Askari aliyemzalisha mama huyo, akiwa amesimama na mmoja wa akinamama ambao pia walijitolea kwa hali na mali katika kufanikisha zoezi hilo,  akiwa amembeba Mtoto huyo mchanga (Dume la Mbegu)



CHANZO- GPL

PRESIDENT KIKWETE TALKS ABOUT U.S PRESIDENT OBAMA VISIT TO TANZANIA


CHUO KIKUU HURIA TANZANIA KUMTUNUKU PhD RAIS OBAMA



Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT),kimepanga kumtunuku Rais wa Marekani, Barack Obama Shahada ya Heshima ya Uzamivu kwa kutambua mchango wake kwa jamii husasani kwenye maendeleo ya kukuza uchumi.


Akizungumza na waandishi wa habari jana,Makamu Mkuu wa chuo hicho,Profesa Tolly Mbwete alisema tuzo hiyo imethibitishwa na Baraza Kuu la Chuo hicho baadaye kupitishwa na Mkuu wa OUT, Dk Asha Rose Migiro.

“Tumeangalia vigezo vyote muhimu ambavyo mtu anastahili kupewa tuzo kama hii na tukaridhika kuwa Rais huyo anastahili kutunukiwa,” alisema Profesa Mbwete.


Kwa mujibu wa Profesa Mbwete, Rais Obama anakuwa mtu wa tano kutunukiwa tuzo hiyo baada ya kutanguliwa na Mwalimu Julias Nyerere, Rais wa kwanza mweusi wa Afrika ya Kusini, Nelson Mandela, Rais wa awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Benjamin Mkapa.


Alisema hadi sasa OUT imetoa shahada saba za heshima, ambapo kati ya hizo mbili walitunukiwa mwanataaluma kutoka Marekani, Dk Jane Goodall na Mhadhiri wa Mawasiliano kutoka nchini Uingereza,David Mellor.

OBAMAS AT THE "DOOR OF NO RETURN." FIRST FAMILY MAKES EMOTIONAL TRIP TO FORMER SLAVING PORT IN SENEGAL FROM WHERE CAPTIVES WERE SHIPPED TO AMERICA.


goree_obama_banner_1932x700.jpg
President Barack Obama spent Thursday afternoon touring a Senegalese island where Africans were shipped across the Atlantic into slavery and he called the visit a 'very powerful moment.' Obama added that, as an African American and an African-American president, the trip gives him even greater motivation to stand up for human rights around the world, and the visit came just hours after he clashed with his Senegalese hosts over gay rights.
SOURCE. www.mailonline.co.uk

Thursday 27 June 2013

RAIS OBAMA APOKEWA KWA SHANGWE NA HESHIMA KUBWA NCHINI SENEGAL, AWASIFU WASENEGAL KWA KUPIGA HATUA KATIKA DEMOKRASI




Rais Obama akiwa na marais mbalimbali  wa nchi za Afrika aliokutana nao huko Senegal.

WASAFIRI TOKA MIKOANI MARUFUKU! KUJA DAR WAKATI WA ZIARA YA RAIS OBAMA. WAZIRI MEMBE



Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe amewashauri watu walioko mikoani kusitisha safari za kuja Dar es Salaam wakati wa ziara ya Rais wa Marekani, Barrack Obama kutokana na wingi wa wageni katika jiji hilo.

Ugeni huo pamoja na ule wa viongozi kumi na moja kutoka nchi mbalimbali duniani watakaohudhuria mkutano wa kimataifa wa Smart Partnership utakaofunguliwa kesho na Rais Jakaya Kikwete kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, umesababisha kuimarishwa kwa ulinzi katika maeneo mbalimbali hasa katika hoteli za kitalii ambazo zimeanza utaratibu wa upekuzi kwa wageni wake.

Akizungumza na katika mahojiano na Redio ya Clouds jana, Membe alisema jiji limefurika kwa wingi wa wageni.
 
“Hoteli na nyumba za wageni zimefurika wageni na magari mengi yamekodiwa. Kwa ujumla, huduma za kijamii zitakuwa shida,” alisema.
 
Rais Obama na mkewe Michelle watawasili nchini Jumatatu na tayari wapambe na maofisa usalama kutokana Marekani wameanza kuwasili. Mbali ya ujio huo, wake wa marais kutoka nchi 14 za Afrika watakaokutana na Laura Bush, mke wa Rais wa zamani wa Marekani, George Bush. Pia Michelle atahudhuria mkutano huo utakaofanyika Jumanne na Jumatano ijayo.


“Jiji la Dar es Salaam litakuwa na mambo mengi kwa hiyo wale wenye kuja kutaka kustarehe wafute safari zao,” alisema na kuongeza: “Kama kuna watu ambao hawapo Dar es Salaam na hawana sababu za kuja mjini waache tu mpaka wageni watakapoondoka kwa sababu jiji la litakuwa limejaa na baadhi ya barabara zitachukuliwa zitumike na wageni hao.”
 
Alisema katika kipindi cha siku tano zijazo, baadhi ya barabara za Jiji la Dar es Salaam zitakuwa na shughuli nyingi na nyingine zitalazimika kufungwa. Barabara itakayofungwa ni pamoja na ile ya Mwai Kibaki na ile ya Bagamoyo itakuwa na shughuli nyingi pia wakati Michelle atakapokwenda Jumba la Makumbusho, Jumanne ijayo.

Wasafiri wa mikoani
Wasafiri wa mikoani wataathirika zaidi Jumanne ijayo wakati Rais Obama atakapokwenda kutembelea mitambo ya kufua umeme ya Kampuni ya Symbion Ubungo.
 
Kituo hicho kipo Barabara ya Morogoro, ambayo ndiyo inayotumiwa na magari yanayoingia na kutoka mikoani.
Rais Obama atakwenda katika kituo hicho yapata saa 4.00 asubuhi na kwa kiasi kikubwa itaathiri magari ya usafirishaji wa mizigo na abiria yatakayokuwa yanatoka na kuingia Dar es Salaam kabla na wakati huo.
 
Na pia tunahabarishwa kuwa Ombaomba wote wamehamishwa katika mitaa ya jiji, haswa wale waliokuwa maeneo ya katikati ya jiji, kufuatia ujaji huo wa Rais Obama.
 

HABARI ZA UMBEYA! MADAM WEMA ALIPOAMKA VIBAYA NA KUZUA TIMBWILI NA WAFANYAKAZI WAKE

Na Siafel Paul

STAA wa filamu za Kibongo asiyekaukiwa vimbwanga, Wema Isaac Sepetu amezua bonge la timbwili kwa wafanyakazi wake wa ndani wa kiume na kike akiwemo mlinzi, Amani linakuletea kisa na mkasa.
Wema Isaac Sepetu akiwa amefura kwa hasira.
Tukio hilo lililonaswa na vifaa vyetu vya kisasa vya kunasia matukio ya mnato na video, lilijiri juzikati nyumbani kwa mwanadada huyo, Kijitonyama, jijini Dar na kusababisha majirani kufaidi sinema ya bure ya matusi ya nguoni.…







CHANZO GPL.

FILAMU MPYA YA AUNT EZEKIEL YAPIGWA STOP BAADA YA KUWA NA VIPANDE VYENYE KUCHOCHEA NGONO



SERIKALI kupitia bodi ya filamu nchini imemkalia kooni mwigizaji, Aunt Ezekiel na kumtaka aondoe baadhi ya vipande vya sinema yake mpya iitwayo Scola vinginevyo haitaruhusiwa kuingia mtaani.


Taarifa kutoka ndani ya bodi hiyo inayosimamia maadili ya sinema za Kitanzania, imeeleza kuwa Aunt aliipeleka filamu hiyo ili ikakaguliwe kama zilivyo taratibu lakini bahati mbaya ikagundulika kuna ‘sini’ tatu ambazo zilitoka nje ya maadili ya mtanzania.
 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!