Friday 28 June 2013

BINTI AJIFUNGUA BARABARANI HUKO NJE KIDOGO YA MOROGORO.

Na Dustan Shekidele, Morogoro

BINTI mmoja aitwaye Josephine Michael mkazi wa Kijiji cha Kiegea nje kidogo ya Manispaa ya Morogoro, Jumatano iliyopita alijifungua barabarani wakati akikimbizwa hospitalini kwa kutumia usafiri wa bodaboda.
Josephine Michael akiwa barabarani baada ya kujifungua.
Tukio hilo lililowashtua watu wengi lilitokea asubuhi kwenye Kituo cha Daladala Cha Nanenane kandokando ya Barabara Kuu iendayo Dar es Salaam.

 Askari wa Barabarani alilazimika kuacha shughuli yake ya kuongoza magari na kusimamisha magari
kumsaidia Binti huyo ambaye alijifungua mtoto wa kiume.


Askari aliyemzalisha mama huyo, akiwa amesimama na mmoja wa akinamama ambao pia walijitolea kwa hali na mali katika kufanikisha zoezi hilo,  akiwa amembeba Mtoto huyo mchanga (Dume la Mbegu)



CHANZO- GPL

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!