Saturday, 21 September 2013

SISI TUNA MAJANGA LAKINI HAWA WENZETU!"...... WANAUME WAWILI WAKAMATWA NA KICHWA CHA MTOTO HUKO NIGERIA...

 




Two men were on Friday in Ibadan paraded by the police for possessing a decomposing human head. One of the men, Seyi Akinola, was arrested in an ambush operation by the police while Ajitoni Ogundeji was named by Akinola as his accomplice in the crime.

Ogundeji, who is a farmer and a hunter, was alleged to have instructed Akinola to bring a human head to prepare a charm that would protect him from gunshot.

Akinola, who is also a hunter, had complained to Ogundeji that he experienced frequent robbery attacks on the road whenever he travelled.

While on hunting expedition at night about two weeks ago, Akinola allegedly saw the corpse of a dead mad woman in a bush.

He later cut off the head and hid it on a tree to decompose.

Ten days later, he returned to pick the head at the place where he kept it but unknown to him, the community had alerted the police after discovering the head on the tree. After walking into the ambush, he was arrested and taken to the police station at Ojoo area of Ibadan. During questioning, he told the police that Ogundeji told him to bring the head to prepare anti-bullet charm. While speaking to journalists at the station, Akinola confessed to the crime.

“I was caught with a human head by the police on Friday morning. I travelled a lot when I was working as a shepherd to a herd of cattle, but there are incidences of robbery attacks on the road. I told Ogundeji about it and he said he could do a charm for me against gunshot if I could get a human head

FEZA KESSY AREJEA BONGO TOKA KWA BWANA SHEMEJI O"NEAL, NA HUU NDIO MUONEKANO WAKE MPYA....


 

Ni ngumu kama kufahamu kama amerudi kimoja ama ndio kaja kuchukua kabisa mizigo yake na kwenda kuishi na prince charming wake Oneal, lakini tunachojua ni kwamba Feza hana tena zile nywele nyekundu zilizokuwa kama utambulisho wake kwenye The Chase,kama tulivyomzowea..

 

SOPHIEMBEYU BLOG NA TIMU NZIMA INAWAPA POLE WENZETU MAJIRANI ZETU WAKENYA KWA TUKIO KUBWA LILILOTOKEA....


JUST IN..........AL-SHABAB IMEKIRI KUISHAMBULIA KENYA, IDADI YA WALIOFARIKI IMEFIKIA 39 MAJERUHI 159.


Kama taarifa imekupita ni kwamba Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amekiri kuwa idadi ya waliofariki inafikia 39 na zaidi ya 150 kujeruhiwa.. hizi picha zimetoka bbcswahili.com

36



35
34
33
38
32
31
30

'Al shabaab imekiri kushambulia Kenya'

http://www.bbc.co.uk/swahili/

http://www.bbc.co.uk/swahili/

WATU 3 WA FAMILIA MOJA AKIWEMO MTOTO WA MIEZI 7 WAMEUAWA KWA KUCHNJWA NA KUNYONGWA HUKO MWANZA LEO

Watu 3 wa familia moja akiwemo mtoto wa miezi 7 wameuawa kwa kuchinjwa na kunyongwa na watu wasiojulikana katika mtaa wa Ihila kata ya Buhongwe Jijini Mwanza usiku wa kuamkia leo

HIVI NDIVYO HALI ILIVYO HUKO NAIROBI BAADA YA WATU WENYE SILAHA KUVAMIA ENEO LA MADUKA KATIKA MTAA WA WESTGATE, NA KUANZA KUFYATUA RISASI , MPAKA SASA WATU 20 WAMERIPOTIWA KUPOTEZA MAISHA....

 

 
 

An injured man is treated outside an upmarket shopping mall, seen background, in Nairobi, Kenya, 21 September 2013. 
A soldier moves to take up a position outside an upscale shopping mall, seen background, in Nairobi, Kenya Saturday 21 September 2013.


Security forces have surrounded the shopping centreShoppers are helped to evacuate the area of an upmarket shopping mall, seen background, in Nairobi, Kenya Saturday 21 September 2013.Dozens of shoppers were given assistance in evacuating the areaTwo women hug outside an upscale shopping mall, seen background left , in Nairobi, Kenya Saturday 21 September 2013.Children and families were taken to safety after the shootings began
A wounded woman is helped to safety after gunmen opened fire in a shopping centre in Nairobi, Kenya. 
A Kenyan woman is helped to safety after shootings in a Nairobi shopping mallA Kenyan woman is carried away from the shopping centre.



A wounded woman is helped to safety after gunmen opened fire in a shopping centre in Nairobi, Kenya

 

Polisi waliojihami kwa silaha wamezingira jengo hilo la Westgate, na kutokana na habari tulizozipata toka BBC, watu 20 wanakadiriwa kupoteza maisha

 
Habari zinasema watu wengi wamenasa ndani ya jengo hilo, na kwamba shughuli za uokoaji zinaendelea.

SOURCE. BBC

BREAKING NEWS........MAJAMBAZI YAMEVAMIA DUKA KUBWA LA WESTGATE KENYA, WAKO NDANI YA JENGO HILO KUANZIA SAA TANO ASUBUHI., POLISI ATAKAYETHUBUTU KUINGIA KUPIGWA RISASI

Breaking News:Majambazi wamevamia duka kubwa la bidhaa la Westagate mjini Nairobi nchini Kenya na kujeruhi watu kadhaa.Mpaka sasa majambazi hao wako ndani ya duka hilo kuanzia saa tano asubuhi leo na haieleweki kinachoendelea ndani.Wanausalama nchini Kenya wako nje ya jengo wakiangalia uwezekano wa kuingia ndani ila kuwaokoa waliondani ya jengo maana kila anayejaribu kusogelea eneo la duka hilo anapigwa risasi.

Majambazi wamevamia duka kubwa la bidhaa la Westagate mjini Nairobi nchini Kenya na kujeruhi watu kadhaa.Mpaka sasa majambazi hao wako ndani ya duka hilo kuanzia saa tano asubuhi leo na haieleweki kinachoendelea ndani.Wanausalama nchini Kenya wako nje ya jengo wakiangalia uwezekano wa kuingia ndani ila kuwaokoa waliondani ya jengo maana kila anayejaribu kusogele anapigwa risasi.

MITINDO MBALIMBALI YA VITENGE.....







The new Day Dream collection from Sika Design. Which dress do u like best? Comment here!






APiF’s list of Top African Designers right now. Check-it out here: http://www.africanprintinfashion.com/2013/02/apifs-list-of-top-african-designers.html


alexandraelle:

 The Heat Free Hair Movement is a protective style initiative started by N-ZO Hair Studios, a Washington DC based salon that emphasizes the importance of protective styling through all of its services. It was inspired by the thousands of women that use sew-in weaves as their protective style of choice, but are limited to styles that require them to heat straighten their hair for the purpose of blending with their style.  This movement not only features pure 100% virgin human hair lines exclusively created for natural hair textures, but serves as a community platform for women to display their heat free styles and connect with an amazing community of natural women. We want our customers to embrace their curls, toss their blow dryers and flat irons in the closet and grow their hair to new heights (and lengths!).
Message from the founder:

“I have always believed in embracing your natural ‘kinks’ and ‘curls’, but also in the benefits of sew-in weaves as a protective style. At my salon, we call it ‘the ultimate protective style’. Being natural for almost a decade, I experienced my greatest length retention during my one-year weave challenge back in 2005. My hair grew over 8 inches! Since then I have maintained both my hair and the hair of my clients through customized regimens and protective styling. Whether you are transitioning without chopping, growing your hair out, protecting it for a period of time, or considering going natural, The Heat Free Hair Movement provides an option that will allow you to embrace your journey with confidence and style. Experience the revitalization of your natural tresses when you GO HEAT FREE!”
–Ngozi Opara
 Heat Free Hair Movement Founder & Owner of N-ZO Hair Studios

Instagram:  @heatfreehair @ngozithestylistWebsite: www.heatfreehair.comtwitter: @heatfreehairFB: facebook.com/heatfreehair
stunning african designs 2013



POLISI TABORA WAKAMATA MAJAMBAZI WATATU,WAHAMIAJI HARAMU KUMI NA MOJA


Watu watatu ambao ni wakazi wa wilaya ya Sikonge ambao wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Tabora kwa tuhuma za ujambazi wa kutumia silaha,watu hao ambao wamedaiwa kuwa wamekuwa wakisumbua wananchi na hata kuwasababishia madhara makubwa kutokana na vitendo vyao vya unyang'anyi wa kutumia Silaha.
Mmoja kati ya makachero wa Jeshi la Polisi wilayani Sikonge akijaribu kuiangalia Silaha aina ya Shortgun waliyoikamata kwa majambazi hao watatu huko wilayani Sikonge

AGNESS MASOGANGE AACHIWA HURU BAADA YA KULIPA FAINI YA SH. MILIONI 4...



Mtanzania Agnes Gerald, maarufu Masogange, ameachiwa huru na Mahakama ya Kempton ya jijini Johannesburg, baada ya kulipa faini ya R30,000 (Sh4.8 milioni) kwa kosa la kubeba kemikali zinazotumika kutengeneza dawa za kulevya. 
  

Wakati Masogange akitozwa faini hiyo mwenzake, Melissa Edward ameachiwa huru na mahakama hiyo, baada ya kukosekana ushahidi wa kumtia hatiani.
 
Msemaji wa Kitengo cha Uchunguzi wa Makosa ya Jinai cha Afrika Kusini(Hawk), Kapteni Paul Ramaloko alisema Watanzania hao wameachiwa huru baada ya kuonekana kuwa hawakubeba dawa za kulevya, bali kemikali aina ya ephedrine.
 

Kwa sheria za Afrika Kusini kubeba kemikali zozote ambazo zimepigwa marufuku ni kosa la jinai kisheria, hivyo mahakama iliamuru Masogange ahukumiwe kwenda jela kwa miezi 30 (miaka miwili na miezi mitano) au alipe faini ya R30, 000 (sawa na Sh4.8 milioni).
 

Hata hivyo, Kapteni Ramaloko alisema mdhamini wa Masogange alilipa nusu ya fedha na kwamba zinazobaki amalizie baadaye.
 

Alisema kutokana na kutomalizia kulipa fedha hizo ataendelea kubaki nchini humo hadi atakapomaliza kulipa nusu ya faini iliyobaki.
 

Masogange na mwenzake walipokamatwa na SARS ilielezwa walikuwa wamebeba dawa za kulevya aina ya

Methamphetamine, lakini Mahakama juzi ilithibitisha walikamatwa na kemikali aina ya Ephedrine, ambayo siyo dawa za kulevya.
 

Wakati Kamishna Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti Dawa za Kulevya nchini, Geofrey Nzowa alipoulizwa na Mwananchi Jumamosi juzi alisema mzigo walioubeba Masogange na mwenzake haukuwa ni dawa za kulevya bali ni kemikali za dawa za kulevya, lakini Msemaji wa Mamlaka ya Mapato ya Afrika Kusini, (SARS), Marika Muller alieleza kuwa timu ya SARS ina uhakika kuwa mabegi sita yaliyokamatwa Julai 5 ni dawa za kulevya aina ya Methamphetamine.

Jana, Muller alipoambiwa kuwa Watanzania hao wameachiwa huru baada ya kulipa faini na mmoja kuachiwa huru kwa kuwa Mahakama imeridhika kuwa hazikuwa methamphetamine bali kemikali aina ya Ephedrine, alirudia tena na kueleza kuwa, mamlaka hiyo ina uhakika na kazi yake na iwapo mahakama imewaachia huru basi yeye hana la kusema zaidi.
 
“Kazi yetu kubwa ni kukamata mizigo haramu inayopitishwa uwanja wa ndege, kama Mahakama imeona kuwa si dawa za kulevya, hatuna la kuongeza. Kikubwa tumemaliza kazi yetu,” alisema Muller kwa kujiamini.
 
Hata hivyo, Nzowa jana akizungumzia kuachiwa huru kwa Watanzania hao, alionyesha kushangazwa jinsi Mahakama ilivyotoa adhabu ndogo.
 
“Hii ni ajabu sana. Kama watu wamebeba mzigo wenye thamani ya Sh6.8 bilioni wanapigwa faini ya milioni nne, hawataogopa kufanya hiyo biashara. Hao watu ni hatari sana,” alisema Nzowa.
 
Alipoulizwa iwapo wakirudi Tanzania wanaweza kushtakiwa, Nzowa alisema kitengo chake hakitaweza kuwashtaki tena kwa sababu wanaweza kujitetea kuwa tayari walishahukumiwa, isipokuwa Mwendesha Mashtaka aliyekuwa akisimamia kesi yao anaweza kukata rufaa.
 
“Iwapo Mwendesha Mashtaka wa huko akikata rufaa kwa kuona adhabu aliyopewa mhalifu huyo ni ndogo, anaweza kufanya hivyo,” alisema Nzowa.
 
Nzowa alisema, inasikitisha kuwa wakati mapambano ya biashara hiyo yakiwa yanaendelea Tanzania, watuhumiwa hao wanaachiwa.
 
“Adhabu waliyopewa ni ndogo hasa wakati huu ambao Tanzania tunachafuka kwa tuhuma hizi. Lazima kitu kifanyike kubadili hali halisi hapa nchini,” alisema.
 
Nzowa alieleza kuwa alikwenda Afrika Kusini tangu Septemba Mosi kuwahoji wasichana hao ambao hata hivyo hawakuweza kusema lolote la kuisaidia polisi.
 
Masogange aliandika kwa maandishi kuwa ni kweli mzigo ulikuwa wa kwake, lakini akasema mdogo wake, ambaye ni Melissa, hajui lolote na alikuwa amemsaidia.
 
Julai 5, mwaka huu Masogange na Melissa walikamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo wakidaiwa wamebeba kilo 150 zilizodaiwa kuwa ni dawa za kulevya aina ya Methamphetamine zenye thamani ya Sh6.8 bilioni.
 
Dawa hizo zilizokuwa zimepakiwa katika mabegi makubwa sita, zinatajwa kuwa ni kiwango kikubwa kukamatwa katika historia ya SARS ndani ya uwanja huo unaotumiwa na mataifa makubwa duniani

Taarifa za kukamatwa kwa wasichana hao zilipamba kurasa mbalimbali za magazeti ndani na nje ya Tanzania, jambo lililosababisha Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe kuchukua hatua za kuusafisha Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere.
 
Baada ya uchunguzi wa Dk Mwakyembe ambao ulibaini kuwapo mchezo mzima uliochezwa wakati Masogange na Melissa walipokuwa uwanja wa ndege.
 
Agosti 17 alitoa agizo la kufukuzwa kazi, Koplo Juliana Thadei, Jackson Manyoni, Yusuph Daniel Issa, Koplo Ernest na Mohamed Kalugwan.
 
Mwakyembe alisema katika hali isiyokuwa ya kawaida mfanyabiashara ambaye hakuwa na tiketi ya kusafiri siku hiyo, baadaye alibadili mawazo hapohapo na kuamua kuondoka siku hiyo kwenda Afrika Kusini na kulipia faini ya dola 60 (Sh96, 000) ili kupata tiketi.
 
Pia Mwakyembe aliliagiza Jeshi la Polisi kushirikiana na Polisi wa Kimataifa (Interpol) kumkamata mfanyabiashara anayedaiwa kumsaidia Masogange kusafirisha dawa za kulevya ambaye alitoweka na mabegi matatu ya dawa hizo huko Afrika Kusini.

TAARIFA MAALUM KWA UMMA KUTOKA WIZARA YA MAMBO YA NDANI



 


Taarifa Maalum Kwa Umma Kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchini Juu ya Operesheni Kimbunga na Usakaji Wahalifu Katika Mikoa ya Kagera, Kigoma na Geita ambao kwa kiasi kikubwa umechangiwa na kuwepo kwa wahamiaji haramu kutoka nchi jirani



JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
 





Simu:  +255-22-2112035/40
        S.L.P.  9223
Nukushi:  +255-2122617/2120486
Barua Pepe:  ps@moha.go.tz
       Dar es Salaam
Septemba 19,2013

---

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete Julai 29, 2013 aliagiza kufanyika operesheni maalum iliyopewa jina la  Operesheni Kimbunga  yenye lengo la kuondoa uhalifu katika mikoa ya Kagera, Kigoma na Geita ambao kwa kiasi kikubwa umechangiwa na kuwepo kwa wahamiaji haramu kutoka nchi jirani.
 

Operesheni hii pamoja na kufanikiwa kuondosha nchini kwa lazima jumla ya wahamiaji haramu 7,819 kuanzia Septemba 6, 2013 hadi kufikia Septemba 17, 2013,   imeweza kushughulikia uhalifu na kufanikiwa kukamata majambazi wa kutumia silaha, majangili, mabomu ya kutupwa kwa mkono , bunduki za aina mbali mbali, Risasi, mitambo ya kutengeneza bunduki aina ya magobole, Sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania, na kibuyu cha maji cha Jeshi hilo.
 

 Jumla ya watuhumiwa wa ujambazi wa kutumia silaha 55 pamoja na mabomu ya kutupwa kwa mkono (8), silaha 47 zikiwemo bunduki aina ya SMG( 4), Shot gun (4), Bunduki aina ya Riffle (2), Bunduki aina ya Mark IV (1), Bunduki aina ya Gobole (37) zimekamatwa wakati wa operesheni Kimbunga hadi kufikia Septemba 17,2013 katika mikoa ya Kagera, Kigoma na Geita.
 

Aidha,   risasi (602) zilikamatwa zikiwemo Risasi (500) za bunduki ya aina ya SMG na SAR, Risasi (20) za bunduki aina ya Mark IV na risasi (82) za bunduki aina ya Gobole, fataki (8), mitambo ya kutengeneza magobole (2), misumeno ya kukata miti ( 9), Mbao (1,516), Magogo (86), na mkaa magunia (111).
 

Aidha, Watendaji wa Operesheni Kimbunga pia wamefanikiwa kukamata jumla ya majangili Watanzania (3), Vipande vya meno ya Tembo (2), Ngozi za wanyama mbali mbali wakiwemo  Nyati (1), Duma (1) na Swala (2). Pia walikamata nyama ya porini,  magunia ya bangi  (6), Gongo lita (86) na lami mapipa (10). 
 

 Wakati huo huo,  Ng’ombe 3,436  wamekamatwa  baada ya wafugaji haramu kutelekeza mifugo hiyo wakati walipozingirwa na timu ya operesheni kimbunga katika mikoa ya Kagera, Kigoma na Geita.
 

Kumekuwepo na tabia ya baadhi ya wamiliki wa mifugo kutoka nchi jirani ambao wengi wao ni matajiri na viongozi serikalini kuwatuma watumishi wao kuingiza mifugo katika ardhi ya Tanzania hususan kwenye hifadhi ya Taifa kwa ajili ya malisho na watumishi hao hupewa silaha kwa ajili ya kujihami wakiwa kazini.  
 

Mifugo imekuwa ikiharibu mazingira na kuleta migogoro ya ardhi katika mikoa hii.

Operesheni Kimbunga itahakikisha inawakamata wahalifu wote wanaotishia amani hususan katika mikoa ya Kagera, Kigoma na Geita. 
 

Aidha, wananchi ambao ni raia pamoja na Raia wenye asili ya nchi jirani wanaowakaribisha na kuwahifadhi wahalifu na wahamiaji haramu watakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria. 
 

Mhamiaji haramu ni raia yeyote wa kigeni aliyeingia na kuishi nchini  bila kufuata utaratibu uliowekwa na  Sheria ya Uhamiaji namba 7 ya mwaka 1995.
 

Utaratibu chini ya Sheria hiyo unamtaka raia wa kigeni anayeingia nchini kuwa na Hati ya kusafiri, kuripoti katika vituo halali vya kuingilia nchini na kujaza fomu za uhamiaji za kuingia nchini.
 

Aidha, Raia wa kigeni anayehitaji kuishi nchini analazimika kuwa na hati za ukaazi itakayomruhusu kufanya shughuli iliyomleta mfano biashara,  matembezi, uwekezaji, Kusoma, matibau, kufanyakazi nakadhalika.
 

Operesheni Kimbunga inayoongozwa na Brigedia Jenerali Mathew Sukambi imeanza rasmi Septemba 6, 2013 baada ya kutoa muda wa wiki Mbili kwa wahamiaji wanaoishi nchini bila kufuata sheria kuondoka kwa hiari.



Taarifa hii imetolewa na  Zamaradi Kawawa, Kiongozi wa  Timu ya Habari na Mawasiliano ya Operesheni Kimbunga. Septemba 19, 2013, Biharamulo, Kagera. Kwa maelezo zaidi piga Simu namba 0754698856, Email; zamaradikawawa@yahoo.com

RAIS KIKWETE AWASHAURI WANASIASA KUWA WA KWELI


 

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete
RAIS KIKWETE ashangazwa na uongozi wa wanasiasa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete ameshangazwa na kiwango cha uongo cha baadhi ya wanasiasa na hasa madai kuwa Rais aliteua wajumbe wa Tume ya Katiba bila kuongozwa na mapendekezo ya wadau mbali mbali waliopendekeza majina hayo.



Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa bado anaendelea kuamini kuwa mchakato wa Katiba Mpya utafikia mwisho wake mwakani, 2014, na hivyo kuiwezesha Tanzania kufanya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 chini ya Katiba Mpya.
Vile vile, Rais Kikwete amesema kuwa hana tatizo na watu wanaopinga sera za Serikali ama hata kumpiga yeye binafsi bali tatizo lake ni wanasiasa na wanaharakati wanaochochea ghasia, fujo na uvunjifu wa amani.

Rais Kikwete aliyasema hayo juzi, Jumatatu, Septemba 16, 2013, mjini San Rafael, California wakati alipokutana na kuzungumza na Jumuia ya Watanzania waishio Jimbo la California, Marekani, wakati alipoanza ziara yake ya siku mbili katika Jimbo hilo ikiwa ni sehemu ya ziara ya Marekani.


Katika hotuba ambako alizungumzia mambo mbali mbali, Rais Kikwete aligusia mjadala wa karibuni Bungeni kuhusu mchakato wa Katiba Mpya na kusema kuwa alishangazwa na madai kuwa yeye kama Rais hakuongozwa na mapendekezo ya wadau wakati anateua Tume ya Katiba.
“Watu wote niliowateua walipendekezwa na wadau mbali mbali zikiwamo taasisi za dini. Yule Mama Maria Kashonda alipendekezwa na Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Mama Mwantumu Malale alipendekeza Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA). Kila kundi ambalo lilipendekeza watu limepata mjumbe katika Tume hiyo wakiwemo walemavu ambao naambiwa nimewasahau,” alisema Rais Kikwete na kuongeza:


“Hivi nyie wanasiasa wenzangu mkikosa hoja mnaongopa hata kwa vitu ambavyo viko wazi kabisa. Tulikubaliana kuwa Rais angefanya uteuzi wa wajumbe wa Tume baada ya kupokea mapendekezo ya wadau mbali na katika mchakato ulioendeshwa kwa uwazi kabisa. Hivyo, ndiyo ilivyofanyika. Sasa uongo wa nini? Kama hakuna hoja ni kwamba hakuna tu na wala uongo hautasaidia.”


Kuhusu kama Tanzania itaweza kupata Katiba Mpya kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, Rais Kikwete amesema: “Ningependa sana, na kwa kweli ni matarajio yangu makubwa, kuwa tuweze kumaliza mchakato wetu mwaka 2014 na tuweza kuwa na Katiba Mpya ili iongoze Uchaguzi Mkuu wetu wa mwaka 2015. Mchakato wetu unakwenda vizuri na wala siyo lazima tuhangaike na Katiba kwa miaka mingi. Muhimu ni ushirikishwaji wa kila mmojawetu.”
Akizungumzia tabia za wanasiasa wa Tanzania kwa jumla na hasa wale wanaochochea chuki na ghasia, Rais Kikwete aliwaambia Watanzania hao:


“Sina tatizo na wanasiasa ama wanaharakati kupinga Sera za Serikali yangu. Hili ni suala la nguvu ya hoja na tunao uwezo mkubwa sana wa kutetea Sera zetu. Na wala sina tatizo na watu kunipinga mimi binafsi. Kinachonipa taabu mimi ni pale wanasiasa na wanaharakati wanapochochea ghasia na kuleta fujo. Kama mtu anataka kuongoza Tanzania si asubiri hadi atakapochanguliwa?”


Aliongeza Rais Kikwete: “Hivi unapochochea ghasia, fujo na chuki na kweli mambo hayo yakatokea na nchi ikateketea, utaongoza nchi ya namna gani? Utaongoza magofu na majivu yatakayobakia baada ya nchi kuteketea?”


Kuhusu mjadala wa karibuni kuhusu kama Rais awe na madaraka ya kuteua wajumbe 166 wa nyongeza ili kuingia katika Bunge la Katiba kujadili Rasimu ya Katiba Mpya, Rais Kikwete amesema kuwa yeye hana taabu kama itabidi ateua basi atateua, lakini kama siyo lazima yeye hana taabu.


“Mimi sina taabu, wakisema niteua basi nitateua. Wakisema nisiteua vile vile sina taabu, isitoshe hiyo itakuwa inanipungumzia mzigo na kazi. Ile kazi yenyewe ya kuteua Wajumbe wa Tume ya Katiba ilikuwa siyo rahisi.”


Rais Kikwete alitumia siku ya pili ya ziara yake katika Jimbo la California kwa kutembelea Jiji la Vallejo ambako alikutana na Meya wa Mji huo, Mheshimiwa Osby Davis, pamoja na madiwani wa Jiji hilo na wafanyakazi wake.


Ziara hiyo ya Rais Kikwete katika Jiji laVallejo, nje ya Jiji la San Francisco, imekuja wakati wa Kumbukumbu ya Miaka 20 tokea Jiji hilo lianzishe uhusiano wa kidada na mji wa Bagamoyo ulioko Mkoa wa Pwani ulioanzishwa mwaka 1993.


Rais Kikwete alitumia muda mwingi wakati wa mkutano na baadaye wakati wa chakula cha mchana na viongozi wa Jiji hilo kujenga hoja ya kuvutia wawekezaji wa Jiji la Vallejo kuwekeza katika uchumi wa Tanzania.


Rais Kikwete pia aliwaelezea viongozi wa Jiji hilo kuhusu historia ya Mji wa Bagamoyo na asili ya jina la mji huo lilitokana na enzi ya watumwa ambako mji uliitwa Bwaga Moyo (Tuliza Moyo Wako).


Rais Kikwete aliondoka mjini San Francisco usiku wa Jumanne, Septemba 17, 2013 na amewasili mjini Washington, D.C. asubuhi ya leo kwa ajili ya ziara ya siku moja katika Mji Mkuu huo wa Marekani.

DAKTARI FEKI ANASWA HOSPITALI YA MUHIMBILI...


Dismas John Macha baada ya kukamatwa jana.
Daktari anayedaiwa kuwa bandia amekamatwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili akiwa na vitambulisho bandia vya mwanafunzi wa  Chuo Kikuu cha Muhimbili cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS) akisomea Shahada ya Pili.

'Daktari' huyo ambaye amekuwa akitafutwa na uongozi wa chuo kwa zaidi ya mwaka alikamatwa jana asubuhi akiwa hospitalini hapo karibu na jengo kilimo kitengo cha meno.
Katika kitambulisho chake cha kupigia kura anatambulishwa kwa jina la Dismas John Macha aliyezaliwa mwaka 1979 Kilimanjaro na anaishi maeneo ya Upanga Magharibi, Dar es Salaam.
Mwandishi, alimshuhudia mtuhumiwa huyo akiwa katika kituo cha usalama cha Muhas  na kupekuliwa na askari Polisi Anthony Mwamatepela na kukutwa akiwa na vifaa vya udaktari.
Baadhi ya vifaa alivyokutwa navyo ni pamoja na koti jeupe la udaktari na stetoskopu ambacho ni kifaa cha kusikilizia mapafu yanavyofanya kazi na mapigo ya moyo.
Pia alikuwa na begi jeusi lenye aina mbalimbali za dawa, vitambulisho na karatasi nyingi, lakini alipoulizwa alidai kuwa hizo ni dawa zake.
Macha alikutwa pia na vitambulisho vitatu tofauti, kimoja kikimtambulisha kuwa mwanafunzi wa Muhas wa Shahada ya Pili ya Udaktari (Masters of Medicine) yenye jina la Macha Dismas kikionesha kusajiliwa kwa namba 60520/2011 na kumaliza muda wake Septemba 30 mwakani.
Kitambulisho kingine kilimtambulisha kwa jina la Macha Rogers anayesoma Shahada hiyo hiyo ikionesha kuwa anamaliza masomo yake mwakani.
Alikutwa pia na kitambulisho kinachomwonesha kuwa mwanafunzi wa Shahada ya Kwanza na kadi ya anuani yenye jina la Amos Nnko ambaye ni Ofisa Rasilimaliwatu wa Chuo hicho.
Akizungumzia alivyomkamata askari wa chuo hicho, Fulgence Semfukwe alisema walimkamata baada ya kupata taarifa za yeye kuwa maeneo hayo na kupanga mbinu za kumkamata.
Alisema saa 4.45 asubuhi  jana alimkuta kwenye jengo la meno na kumwomba kwa nafasi yake ya udaktari  amsaidie tatizo lake na hivyo waongee pembeni, naye bila wasiwasi akakubali.
Alimwuliza anatibu magonjwa gani naye kumjibu anatibu maradhi ya aina nyingi na kumwomba kitambulisho na yeye kumpa cha kwake.
Baada ya hapo alishituka na kudai kuwa ni daktari wa Mwananyamala na amekuja hapo kwa ajili ya kuona wagonjwa wake wa dharura ndipo alipokamatwa na kupelekwa kituo cha Polisi.
Alisema amekuwa akiwachanga kwa muda mrefu kutokana na kuwa kila walipopewa taarifa yuko wodi au sehemu fulani hawakumkuta kwani walipishana naye baada ya kuvua koti na kuweka kwenye begi lake jeusi.
Akizungumza na gazeti hili, Macha limweleza mwandishi wa habari hizi kuwa yeye ni mwanafunzi ambaye anaelewa masuala yote ya matibabu, lakini alifeli chuoni hapo mwaka jana.
Alidai kuwa dawa alizokutwa nazo ni zake kwani ana matatizo katika njia ya mkojo na kifua huku akiamua kufanya hivyo kutokana na ugumu wa maisha.
"Uwezo wa kutibu ninao na nimesoma katika chuo hiki, lakini mwaka jana nilifeli ndiyo maana nikaamua kuwa hivi," alisema.
Ofisa Uhusiano wa Muhas, Hellen Mtui alisema kutokana na kukamatwa na nyaraka akijitambulisha kuwa mwanafunzi wa 'Masters of Medicine', ambaye anaweza kutibu watu hawana uhakika na idadi ya watu ambao ameshatapeli hospitalini hapo.
Kuhusu kusoma Muhimbili, Mtui alikana akisema baada ya kupekua nyaraka za chuo  hawakubaini jina la mwanafunzi wa aina hiyo na katika vyeti vyake bandia vinaonesha kusainiwa na Mkuu wa Chuo aliyekuwapo kabla chuo hakijapanda hadhi na kuwa chuo kikuu.
Mtui alisema baada ya kumkamata na kumpiga picha akiwa na mavazi ya udaktari, kumpekua  na kumhoji walimpeleka katika kituo cha Polisi cha Selander Bridge kwa mahojiano na uchunguzi zaidi.

VISA ZA KIPAUMBELE ZAANZISHWA

Embassy in Kenya - Nairobi - British



 Ili kuimarisha biashara, Ubalozi wa Uingereza nchini umesema, kuanzia sasa Watanzania wanaotaka huduma za viza kwa ajili ya kwenda nchini humo wanaweza kupata huduma hiyo katika kipindi cha muda mfupi kutokana na  kuanzishwa kwa kile kinachoitwa ‘viza za kipaumbele’.
Huduma hiyo ambayo pia imeanza kutumika katika nchi nyingine za Uganda na Kenya inaelezwa kuwa ni moja ya mkakati wa Serikali ya Uingereza kuongeza kasi ya ushirikiano na uwekezaji nchini.
Balozi wa Uingereza nchini, Dianna Melrose alisema uhusiano wa kibiashara baina ya nchi hizi mbili umeimarika zaidi katika miaka ya hivi karibuni hivyo kuanzishwa kwa huduma hiyo mpya kutasaidia kuharakisha kufikia malengo ya kibiashara kwa pande zote.
“Huduma hii ya kipaumbele itahakikisha maombi ya viza yanafanyiwa kazi ndani ya siku tano na mwombaji atatakiwa kulipia kiasi cha Sh250,000,” alisema Balozi Melrose.
Hata hivyo, alifafanua kuwa, pamoja na kuanzishwa kwa huduma hiyo mpya, zoezi la utoaji viza litaendelea kufanywa kwa kufuata sheria za kawaida za uhamiaji.
Viza hizo za kipaumbele zinatazamiwa kutolewa katika makundi mbalimbali ikiwamo wafanyabiashara, wanafunzi na wale wanaokwenda kwa matembezi ya kawaida.
Alisisitiza kuwa viza za kipaumbele zina lengo la kufanya mchakato wa maombi kuwa wa kasi zaidi hasa kwa wafanyabiashara pamoja na wengine ambao watahitaji kufanya maombi ndani ya muda mfupi.
“Tunafanya hivi kutokana na maombi ya wengi, pia kutokana na kukua kwa uhusiano wa kibiashara ili kuleta maendeleo na ajira kwa Watanzania na Waingereza,” alisema Balozi Melrose. 
Kuhusu utoaji viza kupitia ubalozi wake Nairobi, Kenya, Balozi Melrose alisema “Tunafanya hivyo ili kuwa na ufanisi mzuri wa kazi na hakuna upendeleo wowote.”

Friday, 20 September 2013

IJUMAA KAREEM!

 

MSAFIRI KAFIRI!

UGUNDUZI MPYA: WANAUME NAO KUMEZA VIDONGE VYA UZAZI WA MPANGO!


Ni dhahiri kwamba wanaume watashtuka, lakini huenda nao wakashiriki uzazi wa mpango bila upasuaji
Vidonge vya uzazi wa mpango vimezoeleka kutumiwa  zaidi na wanawake pekee, kiasi kwamba ni jambo la ajabu kusikia kuwa wanaume nao wanaweza kuvimeza.
Hata hivyo, watafiti mbalimbali wamefanikiwa kutengeneza vidonge vya uzazi  ambavyo vinazifanya mbegu za kiume  katika mfuko wa uzazi wa mwanamume zisiwe na nguvu ya kuweza kutungisha mimba. Utafiti wa dawa hiyo ambao umewaumiza kichwa wanasayansi kwa miaka mingi umewezesha kupatikana kwa vidonge hivyo ambavyo havina vichocheo kama vile wanavyotumia wanawake ambavyo huingia katika mfuko wa mbegu za uzazi na kisha kuzidhoofisha.
Matokeo ya utafiti huo  ambayo yalichapishwa Agosti mwaka huu yanaonyesha kuwa vidonge hivyo vya uzazi kwa wanaume vitazuia kutunga mimba bila ya kuathiri uwezo wa mwanamume kushiriki tendo la ndoa kama kawaida.
Dk James Brander wa Taasisi ya Dana-Farberanasema utengenezaji wa  vidonge vya uzazi wa mpango kwa wanaume  umekuwa na changamoto kubwa kutokana na  upatikanaji wa dawa ambazo zinaweza kuzuia  mfumo wa utengenezwaji wa  seli za mbegu za kiume.
Dawa hizo ziitwazo JQI zilizotengenezwa katika maabara ya Bradner zinafanya kazi kwa kulenga protini maalumu zilizoko katika korodani  ambazo ni muhimu katika uzazi.
Vidonge hivyo vilichanganywa na vichocheo vya ‘Desogetrel’ ambazo huzuia uzalishwaji wa mbegu za kiume.
Profesa Malise Kaisi wa Chuo Kikuu cha Sayansi ya Tiba Shirikishi Muhimbili (Muhas) ambaye ni Mtanzania wa kwanza kuzalisha watoto kwa njia ya upandikizaji (IVF) anasema ana wasiwasi mkubwa kuhusu dawa hizo kutumiwa kwa wanaume.
“Dawa za uzazi wa mpango ni rahisi kutumiwa na  wanawake kwa sababu wanawake wana mfumo mwepesi kwa dawa kufanya kazi na kuzuia utungishwaji wa mimba,” anasema.
Hata hivyo, Profesa Kaisi anahisi  kwa wanaume itakuwa hatari kwao kutumia dawa hizo kwani kunaweza kusababisha hata kuua kabisa uzalishwaji wa mbegu.
“Wanaume wana maumbile tofauti na mwanamke. Korodani za mwanaume ni kama kiwanda kinachofanya kazi usiku na mchana. Kwa siku moja mwanamume anazalisha mbegu milioni 10,” anafafanua Prof.  Kaisi.
Katika kuzifanyia utafiti, panya dume alipewa dawa hizo, kisha akawekwa pamoja na mwenza wake ambapo  licha ya kujamiiana hata baada ya miezi kadhaa  panya jike hakupata mimba
 Utafiti huo ulibaini kuwa pamoja na kuzuia uzalishwaji wa mbegu, vilevile dawa hizo zilionekana kuwa hazina madhara yeyote kwa kuwa hazina mchanganyiko wa vichocheo vya aina yoyote.
“Hazikuwa na madhara ya vichochezi (hormone). Mwanamume atakayezitumia hatabadilika tabia au mwili kupata mabadiliko yeyote yale” anasema Dk Martin Matzuk, mtafiti mwingine wa dawa hizo.
Dk Matzuk anasema hakuna kinga yeyote nyepesi ya uzazi wa mpango kwa wanaume iliyowahi kugunduliwa tangu kugunduliwa kwa mipira ya kiume miongo kadhaa iliyopita.
Inaelezwa kuwa utafiti huo  ni mkubwa na utakaoleta mapinduzi katika uzazi wa mpango baada ya vidonge vya uzazi kwa wanawake kuonekana na upungufu kadhaa.
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake, Cyriel Massawe wa Chuo  Kikuu cha Sayansi ya Tiba Shirikishi Muhimbili , anasema iwapo kweli dawa za uzazi wa mpango zitagunduliwa basizitasaidia wanandoa kujadili namna bora zaidi ya kupanga uzazi.
“Wenza wanapokuwa na uchaguzi wa kutosha wa namna ya kupanga uzazi inawasaidia wote wawili. Kwa mfano kama mama ana matatizo kadhaa, basi baba atachukua jukumu la kutumia vidonge ili kupanga uzazi,” anasema Dk Massawe.
Anasema kwa sasa wanaume wana njia moja tu ya kupanga uzazi ambayo ni mipira ya kiume hivyo basi iwapo njia nyingine zaidi zimepatikana basi itasaidia.
Dk Massawe anasema vidonge vya uzazi wa mpango kwa wanaume  bado vina changamoto kwa sababu ya mfumo wa uzazi wa mwanamume.
“Zile dawa zinatakiwa zikazuie uzalishwaji wa mbegu kwa wanaume kwa hiyo ili kuingilia mfumo wa uzalishwaji na  pindi mwanamume atakapoacha kutumia awe kama kawaida…ni changamoto” anasema.
Hata hivyo, Dk Massawe anasisitiza kuhusu ushirikiano wa wenza katika kupanga uzazi na kusema kuwa, ni suala linalohitaji watu wawili kujadiliana ili kujua ni njia ipi na salama ya uzazi wa mpango.
 Anaongeza kuwa wenza wanapopanga uzazi itawasaidia kuimarisha afya zao, za watoto na hata kupunguza mzigo wa majukumu ambayo hayakutarajiwa.
Utafiti mwingine unaofanana na huu ulifanywa mwaka 2010 ambapo wanasayansi waliwauliza wanawake na wanaume iwapo wanaume wanaweza kutumia dawa za uzazi wa mpango  pindi zitakaposhauriwa na 
 Katika utafiti huo ulioongozwa na Dk Judith Eberhardt wa Chuo Kikuu cha Masuala ya Jamii,wanaume, 140 na wanawake 240 waliulizwa kuhusu matumizi ya vidonge vya uzazi wa mpango kwa wanaume.
 Hata hivyo matokeo ya utafiti yalionyesha kuwa ingawa wanaume wote walisema watafurahi kutumia vidonge hivyo lakini wanawake walipata hofu iwapo wenza wao watakubali kutumia vidonge hivyo au kuvitumia inavyotakiwa ili kuimarisha uzazi wa mpango.
 Katika utafiti huo, wanaume walio kwenye mahusiano ya kudumu walitoa maoni ya kuvikubali vidonge hivyo huku wale walio katika mahusiano ya muda mfupi waliikosoa njia hiyo ya uzazi wa mpango.
Mei 2009, wanasayansi wa Chuo Kikuu cha Tiba cha Manchester, Uingereza walitumia wanawake na wanaume kuzifanyia utafiti njia za uzazi wa mpango kwa wanaume kujua iwapo zinafanya kazi ipasavyo na zina manufaa.
 Watafiti hao waliwaambia wenza walioshiriki katika utafiti huo kuwa wanaume pekee watumie njia za uzazi wa mpango huku wanawake wakiambiwa kutotumia njia yeyote ili kupima iwapo njia za uzazi wa mpango zinafanya kazi kwa ubora au la.
Hata hivyo, wanaume kadhaa  nchini walioulizwa  iwapo watakubali kutumia njia yeyote ya uzazi wa mpango ikiwemo vidonge na wanaume wanane kati ya kumi, walikataa kutumia njia yeyote ile.
 Mmoja wao,     Edwin Mnzeru anasema, yeye na mke wake hawawezi kutumia njia ya uzazi wa mpango  ya vidonge, mipira ya kiume, wala ya kitanzi   kwa sababu  zina madhara kiafya na ni kinyume na dini.
chanzo:mwananchi
 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!