Pages

Saturday, 19 July 2014

WATANZANIA 54 KUPATIWA AJIRA MITAMBO YA KUCHAKATA GESI

Balozi wa China Tanzania, Lu Youqing

 Watanzania 54 wanatarajia kupata ajira katika mradi wa ujenzi wa mitambo ya kuchakata gesi katika kijiji cha Madimba Wilaya ya Mtwara, unaotarajiwa kukamilika Desemba mwaka huu. 
Hayo yalisemwa jana kijijini hapo na Mkurungezi wa Masoko na Uwekezaji kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC), Joyce Kisamo.
Akielezea hatua za ujenzi huo, mbele ya Balozi wa China nchini Tanzania, Lu Youqing, alipotembele  kijijini hapo, kwa ajili ya kukagua ujenzi huo, alisema kuwa, kukamilika kwa mradi huo kutaleta mabadiliko katika uwekezaji Mtwara, na taifa kwa ujumla na kuwaomba Watanzania wenye sifa kujitokeza kuomba ajira ili kujinufaisha na rasilimali gesi.
Awali Balozi wa China Lu Youqing, aliwashukuru makandarasi wa Tanzania  wanaoendesha shughuli za ujenzi huo kwa kushirikiana na makandarasi wa China.
“Ushirikiano wanatoa makandarasi kufanikisha ujenzi huu ni dhahiri kuwa China na Tanzania ni zaidi ya marafiki, tuendelee kudumisha ushirikiano huu ili tujenge nchi zetu,” alisema.

No comments:

Post a Comment