Akielezea hatua za ujenzi huo, mbele ya Balozi wa China nchini Tanzania, Lu Youqing, alipotembele kijijini hapo, kwa ajili ya kukagua ujenzi huo, alisema kuwa, kukamilika kwa mradi huo kutaleta mabadiliko katika uwekezaji Mtwara, na taifa kwa ujumla na kuwaomba Watanzania wenye sifa kujitokeza kuomba ajira ili kujinufaisha na rasilimali gesi.
Awali Balozi wa China Lu Youqing, aliwashukuru makandarasi wa Tanzania wanaoendesha shughuli za ujenzi huo kwa kushirikiana na makandarasi wa China.
“Ushirikiano wanatoa makandarasi kufanikisha ujenzi huu ni dhahiri kuwa China na Tanzania ni zaidi ya marafiki, tuendelee kudumisha ushirikiano huu ili tujenge nchi zetu,” alisema.
No comments:
Post a Comment