Pages

Saturday, 19 July 2014

PINDA AAHIDI KUCHANGIA UJENZI WA KITUO CHA KULELEA WATOTO WENYE ULEMAVU WA NGOZI(ALBINO)

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
Waziri  Mkuu, Mizengo Pinda, ameahidi   kutoa Shilingi milioni tano kufanikisha  ujenzi   wa kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu   wa ngozi (albino) katika kijiji cha  Lukungu,  wilayani  hapa. 
Waziri wa Mifugo na  Maendeleo ya  Uvuvi, Dk. Titus  Kamani, alipotembelea ujenzi wa kituo hicho jana, alisema kuwa Waziri mkuu ameahidi kutoa fedha hizo baada ya kuguswa  na umuhimu wa kuwepo kwa kituo hicho. Alisema kituo hicho kitapunguza hofu  miongoni mwa watoto wenye ulemavu   kutoka mikoa ya Kanda ya ziwa. "Kabla ya kuja kutembelea ujenzi wa kituo  hiki nimezungumza na waziri mkuu, Mizengo  
Pinda...baada  ya kumueleza  kwa kina  juu  ya malengo ya kituo  hiki ameguswa sana,  na  hivyo   ameahidi  kuchangia   shilingi  milioni  tano," alisema Dk. Kamani.
 
Dk Kamani alisema, ujenzi huo umeshaanza na unatarajiwa kukamilika kabla ya mwishoni  mwa mwaka kesho kwa gharama ya zaidi ya Sh. bilioni 1.5.
 
Alisema kituo hicho kitakuwa na uwezo kwa  kuhifadhi watoto 100 kwa wakati mmoja    watakaopewa huduma ya masomo bure.
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment