Wednesday 21 February 2018

Mtoto wa miaka sita afariki akiombewa kutoa mapepo

Image result for ARRESTED
Geita. Mtoto wa miaka sita amefariki dunia akiombewa mlimani alikopelekwa kutolewa mapepo, huku mama yake mzazi akishikiliwa polisi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo akizungumzia tukio hilo amesema lilitokea Februari 18,2018 saa tano asubuhi katika mlima Gambiwe.

Amesema mama wa mtoto Neema Petro (25) na mke mwenzake Raheli Musa (25) walikwenda mlimani na mtoto huyo kwa ajili ya maombi na kufunga.

Kamanda amesema wanawake hao wakazi wa kijiji cha Bukulu wilayani Nyang'hwale wanashikiliwa kutokana na kifo cha mtoto Frank Bariki (6), ambaye mwili wake umekutwa na majeraha shingoni na kwenye mbavu.

Mwananchi

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!