Friday, 15 April 2016

MFANYABIASHARA AHUKUMIWA KWA KUTOTOA RISITI


Mfanyabiashara Manji Nariadhara leo amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela au kulipa faini ya Sh2.2milioni baada ya kupatikana na hatia ya kuuza bidhaa bila kutoa risiti kwa mteja.

Nariadhara ambaye ni mmiliki wa duka la bidhaa za plastiki amehukumiwa kifungo hicho katika Mahakama ya wilaya ya Ilala baada ya kukiri shtaka linalomkabili.

Hata hivyo, mshtakiwa huyo alifanikiwa kulipa faini na hivyo kukwepa kifungo cha miaka mitatu jela.
Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama hiyo Juma Hassan amesema kwa kuwa mshtakiwa amekiri mahakamani shtaka la kuuza bidhaa bila ya kutoa risiti kwa wateja, hivyo anastahili kifungo cha miaka mitatu jela au kulipa faini ya Sh3milioni.
Awali, kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo, wakili wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) Harold Gugami, aliiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa mshtakiwa huyo ili iwe fundisho kwa watu wengine wasiotoa risiti za faida ya mauzo kwa kutokuwa na mashine.
Hata hivyo, mahakama hiyo ilitoa nafasi kwa mshtakiwa kujitetea kwa nini asipewe adhabu na kwamba, Nariadhara aliiomba mahakama kumpunguzia adhabu kwa kuwa hali ya baba yake ni mgonjwa naye ndiye anayetegemewa kuiangalia familia hiyo.
Juzi , mshtakiwa huyo ambaye ni mmiliki wa duka hilo la vifaa vya plastiki alishindwa kufika mahakamani hapo kwa madai kuwa ni mgonjwa na badala yake alikuja meneja mauzo wa duka hilo, Deepesh Manji.
Kutokana na mmiliki kushindwa kufika mahakamani hapo, Mahakama iliamuru mmiliki huyo aletwe mahakamani kwa ajili ya kusomewa shitaka hilo.
Hata hivyo, baada ya kufika mahakamani hapo jana mmiliki huyo alishindwa kuendelea kusikiliza kesi hiyo kutokana na hali yake kiafya kutokuwa nzuri na hivyo shitaka hilo kubadilishwa na kusomewa meneja huyo ambaye ni mtoto wa mmiliki.
Wakili wa TRA, Gugami alisema Sheria ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kifungu cha Sheria ya Usimamizi wa kodi namba 86 ya mwaka 2015 inatoa kibali cha kesi kubadilisha mshtakiwa.
Katika hati ya mashtaka, inadaiwa kuwa Machi 17, mwaka huu eneo la Mchikichini, Kariakoo wilaya ya Ilala, katika duka la Nariadhara, mshtakiwa huyo alishindwa kutoa risiti kwa mteja Hussein Yasin baada ya kununua bidhaa yenye thamani ya Sh8,100.
MWANANCHI.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!