Friday, 15 April 2016

WENYE ULEMAVU WA KUSIKIA WALALAMIKA RUSHWA YA NGONO

WANAWAKE wenye ulemavu wa kutosikia (viziwi) wamelalamikia rushwa ya ngono wakati wa kutafuta ajira na wanapotaka matibabu.


Walisema hayo wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kupambana na rushwa, yanayotolewa na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa Tanzania (Takukuru) kwa jamii ya watu hao mkoani hapa kwa kuwa wanao ni waathirika wakubwa.
Mratibu wa chama cha watu wenye ulemevu wa kutosikia, Francis Mbiso, alisema viziwi wamekuwa wakipata taarifa nyingi za masuala ya rushwa, lakini wanashindwa kuziwasilisha kwa wahusika kutokana na kutokuwa na uelewa wa kutosha.
Ofisa Takukuru, Mercy Marco, alisema taasisi hiyo imeendelea kutoa elimu ya rushwa kwa makundi mbalimbali ya jamii wakiwamo walemavu ili waweze kusaidia taasisi hiyo kwa kutoa taarifa kwa njia ya ujumbe ili kusaidia kupunguza kupokea ama kutoa rushwa katika maeneo wanayopata huduma.
Alisema mapambano dhidi ya rushwa si suala la Takukuru pekee, kila mmoja anatakiwa kushiriki kikamilifu na dhati kwa kutoa taarifa itakayosaidia jamii kuendelea kupambana.
Alisema walemavu hao ni walimu ambao watasaidia kueleimisha wenzao, kwani wakifundishwa makosa mbalimbali ya rushwa wanamchango mkubwa wa kusaidia taasisi ndo maana wanashiriki kuweka mikakati ya pamoja.
Baadhi ya walionufaika na mafunzo hayo akiwamo, Asha Fungo, alisema yatasaidia viziwi kuwa na uwezo wa kupata mbinu ya kupambana na rushwa ambayo imetawala katika maeneo ya Mkoa wa Morogoro.
Alitoa mfano wanapoombwa rushwa na kukataa, hujikuta wakikosa huduma.
Walemavu hao waliahidi kuzuia rushwa kwa kutoa taarifa kwa mamlaka husika.
NIPASHE

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!