Friday, 15 April 2016

Mlinzi ajeruhiwa kwa risasi migodi ya Tanzanite


MIGOGORO ya ‘mitoboano’ katika migodi ya Tanzanite, imechukua sura mpya, baada ya mlinzi wa mgodi wa Joseph Mollel, maarufu kama Papa King kupigwa risasi.


Akizungumza katika wodi ya majeruhi ya Hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru, mlinzi wa mgodi huo, Joseph Thomas (20), alisema alipigwa risasi na mmiliki wa mgodi jirani.
Alisema akiwa chini ya mgodi huo Jumanne wiki hii, wachimbaji wa mgodi jirani walitoboa hadi kwenye mgodi wao na kujaza udogo.
Alisema baada ya kutoka nje ya mgodi ugomvi kati yao ulizuka na ulipozidi mmliki wa mgodi huo (jina limehifadhiwa), aliingilia kati na baadaye akampiga risasi.
Alidai kuwa alilengwa kichwani, lakini alipokwepa bahati nzuri risasi hiyo ilimpata mguuni.
Alisema tukio hilo lilitokea saa 7 mchana na baada ya meneja wa mgodi huo kutoa taarifa polisi, alifikishwa hospitalini saa 6: 00 usiku.
Akizungumzia tukio hilo, Meneja wa mgodi huo, Elikana Sanayo, maarufu kama Nyundoo, alisema baada ya tukio hilo alitoa taarifa polisi na ofisi ya madini na kumpeleka hospitali kwa matibabu.
Daktari aliyempokea, Abraham Maro, alithibitisha jeraha alilopata mlinzi huyo lilitokana na risasi.
Alisema baada ya uchunguzi wa kitabibu tuligundua jeraha hilo lilitokana na risasi.
Hata hivyo, alisema uchunguzi ulionyesha risasi hiyo haikuvunja mfupa wa mguu wake.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Daud Ntibenda, akizungumzia na maofisa watendaji wa kata, mitaa na wenyeviti wa serikali za mitaa hivi karibuni, alisema amesitisha utoaji wa silaha hadi zoezi la uhakiki utakapokamilika.
Alisema wakazi wengi jijini hapa wamemilikishwa silaha kwa kudanganya kwamba ni wafanyabiashara ya madini.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!