MATESO! Mtoto aitwaye Chacha Robert (15), (pichani), mkazi wa Musoma, Mara anateseka na ugonjwa wa ajabu wa kuota magamba kama ya nyoka sehemu ya mwili hali inayomsababishia kutengwa na jamii.
Taarifa kutoka kwa mtu wa karibu na familia yake zinaeleza kuwa, Chacha alizaliwa hivyo na mama yake mzazi alifariki dunia saa chache baada ya kujifungua.
Mtu huyo aliendelea kuliambia Amani kuwa, kutokana na imani ya watu wa maeneo hayo, ugonjwa wa Chacha unaaminika kuwa, unatokana na imani za kishirikina.
“Wao kama Wakurya waliamini kwamba mama yake aliona chatu wakati akiwa mjamzito ndiyo maana mtoto akazaliwa hivyo.
“Chacha kwa sasa anasoma kidato cha kwanza kwa shida. Wanafunzi wenzake wanamnyanyapaa na kumuoneshea vidole kila anapopita,” alisema mtu huyo ambaye ndiye mwangalizi wa karibu wa maisha ya Chacha.
Akaendelea: “Tulimpeleka hospitali, daktari akasema ugonjwa huo unaitwa Ichthyosis ambao unafanana na Albinism anavyozaliwa. Na msaada anaouhitaji ni kubadilisha nguo mara kwa mara na kula vyakula vya kiasili.
“Kwa sasa, Chacha anaishi na baba yake na babu yake na hali yao kiuchumi si nzuri na ndiyo maana tumewaomba nyie Global mtusaidie.”
Watanzania kutoa ni moyo, kwa yeyote atakayeguswa na habari hii anaweza kuwasilisha mchango wake kupitia simu ya mkononi ya mtu anayemwangalia Chacha kwa karibu ambayo ni 0759665555.
Picha kwa hisani ya Flora Show.
No comments:
Post a Comment