Thursday, 17 September 2015

Mtoto adhaniwa kupeleka bomu shuleni

Image copyrightANIL DASH
Image captionKijana Ahmed Mohamed aliyekamatwa akihofiwa kupeleka bomu shuleni
Raisi Barrack Obama amemualika ikulu mvulana wa kiislamu mwenye umri wa miaka 14 mara baada ya kushikiliwa na polisi kwa muda baada ya kupeleka shuleni saa aliyoitengeneza mwenyewe nyumbani na mwalimu wake kudhania kuwa ni bomu.


Kupitia ukurasa wa twitter Raisi Obama alimsifu Ahmed Mohamed kwa saa yake hiyo na kuwataka watoto wengine kuhamasika na kufurahia sayansi kama Ahmed.
Hapo jumatatu kijana huyo alishikiliwa na polisi baada ya mwalimu wake alipotoa taarifa polisi kuhusu chombo alichokuja nacho shuleni.
kikundi cha kiislamu nchini Marekani kilizungumzia suala hilo kuwa kijana huyo alikamatwa kwa kuwa ana Imani ya Kiislamu.
Taarifa ya kukamatwa kwake kulileta hisia tofauti katika mitandao ya kijamii.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!