Thursday, 17 September 2015

ONA UNENE UNAVYOTUHARIBU! SOMA ZAIDI NINI CHA KUFANYA KUEPUKA/ KUPUNGUZA UNENE




Kwanza kabisa napenda kuwashauri watu
wanene wasitumie vidonge/madawa ya
kiwandani kwa lengo la kupunguza unene,
kwani vidonge vina athari zake mwilini
ukizingatia kuwa vina kemikali ambazo baadhi
hubakia mwilini na kutengeneza sumu.
Watu wanashauriwa kutumia vitamini itokanayo
na matunda na mbogamboga. Aidha, kwa mtu
mnene kushinda na njaa siyo dawa au tiba
sahihi ya kupunguza unene. Mtu anayetaka
kupunguza unene/uzito ni vema akazingatia
misingi ifuatayo:
Punguza kula chumvi nyingi
maana chumvi inatunza maji
mwilini ambayo pia yana
mchango mkubwa katika
kuongeza uzito wa mwili. Kwa
kuacha kula chumvi nyingi maji
yataweza kupungua mwilini kwa
njia ya mkojo au jasho.
Ongeza kula vyakula vyenye
madini ya potasium, calcium, na
magnesium ambapo madini hayo
yanapatikana kutoka kwenye
mbogamboga mbichi na matunda
au maziwa ya soya.
Kula vyakula vyenye wanga,
punguza vyakula vyenye mafuta
na protini.
Kunywa maji mengi kiasi cha lita
2 kwa siku na kwa kila siku.
Fanya mazoezi ya mwili/viungo
japo kwa dakika 30 hadi 60 kila
asubuhi. Kutembea ni mojawapo
ya mazoezi.
Katika kuongezea vitu hivyo hapo juu, mlengwa
anashauriwa pia kutumia;
Asali kijiko kimoja na
kuchanganya nusu ndimu au
limao kwenye maji yenye
uvuguvugu kiasi cha glasi moja
na kunywa mara kwa mara.
Matumizi ya cabbage pia
yamethibitika kuwa na mchango
mkubwa katika kupunguza unene
kwani kemikali zilizomo ndani
yake zinasaidia kuzuia wanga na
sukari kubadilishwa kimfumo na
kuwa mafuta ambayo ndicho
chanzo cha unene wa mwili.
Ulaji wa nyanya fresh kati ya moja
au mbili kila siku asubuhi kama
kifungua kinywa kwa miezi
kadhaa nako kunachangia
kupunguza unene, na ni njia
salama sana ya kupunguza
unene.
Kunywa glasi mbili za maji ya
uvuguvugu kila siku asubuhi mara
baada ya kuamka kunasaidia
kupunguza unene.
Aidha mtu mnene anaweza kutumia diet rahisi
ifuatayo ili kupunguza unene;
1. Asubuhi, kunywa juisi ya matunda fresh au
kula matunda na kipande cha mkate
usiopakwa siagi.
2. Mchana, kula vegetable salad na slice 2 za
mkate pamoja na matunda au juisi.
3. Usiku, kula fruit salad au supu ya
mbogamboga.




UPO UFANYAJI MAZOEZI WA AINA MBILI


5-MAZOEZI YA MWILI NA VIUNGO
Mazoezi ni mfalme wa kupunguza unene.
Ukiwauliza wengi watakuambia wanafanya kazi ngumu za sulubu (wanachuruzikwa jasho) kwa hiyo hayo ni mazoezi. Ila kazi na mazoezi ni vitu viwili tofauti. Ingekuwa kufanya kazi ni mazoezi basi kusingekuwa na wastani mfupi wa maisha kwa maskini hasa sisi Waafrika.
Wengine watadai kwamba walipokuwa wadogo shuleni walifanya mazoezi sasa wamekuwa watu wazima (miaka 40 kuendelea) kwamba eti mazoezi ni suala la ujana; kumbe kadri unavyokuwa ki umri ndivyo kadri unavyotakiwa kufanya mazoezi na kujitazama zaidi kiafya.
Watazame Wachina na Wajapani wanavyoishi maisha marefu.
Mazoezi ni shughuli inayokufanya kwanza uheme (mapafu na moyo kwenda kasi), viungo na mifupa kujinyoosha (stretching), kutoka jasho na usafishaji wa damu. Mazoezi yanayosaidia haya ni pamoja na kutembea kasi, kukimbia, kuogelea, michezo mbalimbali ya riadha (kama mpira wa miguu, nyavu, kikapu, mikono, nk); michezo ya kupigana na kujilinda yaani masho ati(karate, kung fu, judo, capoeira, krav maga, jiu jitsu, systema, kickboxing, thai boxing, kempo, kalari payatu, aikido, nk) …
Ni muhimu mwanadamu ufanye mazoezi makali ya viungo mara mbili tatu kwa juma. Si vizuri kufanya kila siku kwani misuli na mishipa inahitaji kupumzika na kukua.







KUFUNGA
Ufungaji ninaouongelea ni ufungaji wa kutokula kabisa kwa saa 24, 36 hadi 48 kuendelea…
Ufungaji ni nini?
Kama mashine yeyote mwili wa mwanadamu unahitaji kupumzika na kujisafisha. Hata tukiwa tumelala bado viungo mbalimbali mwilini vinafanya kazi. Kwa hiyo faida ya kwanza kabisa ya kufunga ni kuupumzisha mwili kama mfanyakazi yeyote anapokwenda likizo.
Faida ya pili ya kufunga ni kusafisha mwili kutokana na uchafu ambao haukutoka (kinyesi hakitoi mabaki yote toka utumbo mkubwa), dawa na takataka za mazingira tunayoyavutia hewa, virusi au kuyanywa katika maji na vyakula mbalimbali na pia uchafu wa hisia, yaani hasira, huzuni, nk.
Kuna ufungaji wa aina mbalimbali.
1-Kufunga kwa kunywa maji tu, saa 24 kuendelea…
2-Kufunga kwa kutokunywa maji au kula chochote, saa 24 kuendelea…
3-Kufunga kwa kula tu matunda au mboga zilizopondwa kama karote, matango nk, saa 24 kuendelea…
Ufungaji huu unatakiwa ufanywe kwa mpangilio. Kitu muhimu si tu kufunga bali NAMNA unavyofungua. Ukianza kula tena, unaanza taratibu. Kawaida ni vizuri kuanza na maji, kikombe au bilauri ya kwanza taratibu. Subiri tena nusu saa, bilauri nyingine, halafu hadi ya tatu, halafu ndiyo matunda yasiyo ya chachu, na kadhalika. Kuanza kufungua kwa kunywa chai ya maziwa, uji au vyakula vingine vya wanga hakusadii sana mfungo huu.
Maana lengo lake ni kusafisha mwili.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!