Thursday, 17 September 2015

Bawacha yawataka wanawake wasikubali kudanganyika na zawadi za msimu.

Baraza la wanawake wa chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA limewataka wanawake wa mkoa wa Geita kutokudanganyika kwa zawadi za msimu za tisheti na kanga na kusahau  kero zinazowakabili  kwa muda mrefu badala yake wapime hatima ya maisha yao kwa kipindi cha miaka mingine mitano  baada ya uchaguzi.



Wakizungunza na wanawake wa mkoa wa geita naibu katiku mkuu wa baraza la wanwake wa chama cha demokrasia na maendeleo chadema kunti yufu na mke wa mgombea urais  kupitia  umoja wa vyama vinavyounda ukawa mama regina lowasa wamesema  kwa zaidi ya miaka 50 changamoto za wanawake bado ni kubwa hivyo wanahitaji kufanya mabadiliko  mfumo wa kisiasa kwa kuwapa ridha viongozi ambao wanaguswa na maisha magumu ya wanawake  hasa waliovijijini.
 
Kwa uoande wao wanawake wa koa wa geita wakizungumza katika mkutano huo wameeleza cangamoto kubwa  ni kero ya maji ambapo wanalazimika kutumia maji ya mito ambayo yanachanganyika na mabaki ya madini yanayochimbwa katika migodi mbalimbali na hivyo kuomba endapo watapata ridhaa  katika serikali ya mabadiliko kupitiaukawa  kero hizo zitafutiwe majibu. 

ITV.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!