JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA
MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA
Simu: 255-22-2114615,
211906-12
Barua
pepe: nje@nje.go.tz
Barua
pepe: gcu@nje.go.tz
Tovuti :
www.foreign.go.tz
Nukushi: 255-22-2116600
|
20 KIVUKONI FRONT,
P.O. BOX 9000,
11466 DAR
ES SALAAM,
Tanzania.
|
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Safari za Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete Nje ya Nchi
Wizara imesikitishwa na taarifa za
uongo zilitolewa katika vyombo vya habari kuwa Mhe. Jakaya Kikwete, Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uongozi wake wa miaka 10 ametumia
Shilingi trilioni 4 kwa ajili ya safari za kikazi nje ya nchi, ambazo ni wastani
wa bajeti nzima ya wizara kwa miaka mitano (5).
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Kimataifa inapenda kutoa ufafanuzi kuwa tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete aingie madarakani mwaka 2005, kiasi
kikubwa kabisa cha bajeti kuwahi kutengwa kwa ajili ya safari za Viongozi Wakuu
yaani Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu ni shilingi bilioni 50 ambazo
zilitengwa kwa Mwaka wa Fedha 2014/2015 kwa ajili ya Idara ya Itifaki. Kwa
miaka mingine yote wastani umekuwa ni kati ya shilingi bilioni tano hadi 25
kulingana na mahitaji ya idara hiyo.
Ifahamike kuwa kiasi hicho cha
shilingi bilioni 50 ni bajeti nzima ya Idara ya Itifaki, ambapo kuna fungu maalum
kwa ajili ya ziara za viongozi. Fungu hilo linagharamia makundi makuu matano
kama ifuatavyo:
1.
Kundi la Rais wakiwemo
Wasaidizi, Mawaziri au Wakuu wa Taasisi na Walinzi;
2.
Kundi la Makamu wa Rais
wakiwemo Wasaidizi, Mawaziri au Wakuu wa Taasisi na Walinzi;
3.
Kundi la Waziri Mkuu
wakiwemo Wasaidizi, Mawaziri au Wakuu wa Taasisi na Walinzi;
4.
Kundi la Wakuu wa Nchi na
Serikali kutoka nje ya nchi wanapotembelea Tanzania; na
5.
Kundi la Wajumbe Maalum
wanaokuja nchini kuleta taarifa muhimu kwa Rais.
Makundi yote haya hugaramiwa na
Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje ndani ya bajeti ya Idara ya Itifaki
kifungu cha Ziara za Viongozi.
Aidha uandaaji wa bajeti ya Wizara
chini ya Idara ya Sera na Mipango unahusisha wadau wengine nje ya Wizara kama
vile Kamati ya Bunge ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na hupitishwa kila
mwaka na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Tunapenda kuwaatahadharisha wananchi
juu ya watu wanaotoa taarifa za uongo kwa madhumuni ya kujenga chuki dhidi ya Serikali. Ikumbukwe kuwa ziara za viongozi
zinazoratibiwa na Wizara ya Mambo ya Nje zina mafanikio makubwa kwa nchi na
Watanzania kwa ujumla.
Wizara inaandaa taarifa ya ndefu ya
utekelezaji wa majukumu ya Wizara, changamoto na mafanikio yaliyopatikana ndani
ya kipindi cha miaka kumi ya uongozi wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete ambayo
itatolewa kwa umma kwa lengo la kutoa elimu zaidi.
MWISHO.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya
Serikali kwa Umma,
Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa,
17 Septemba 2015
No comments:
Post a Comment