Na katika futari hizi hakikisha unachagua vyakula vyenye lishe, maana Mungu alituambia tufunge ili tupate afya. Lakini kutokana na uroho ama ulafi, wengi huchanganya vyakula vingi vya wanga, nyama na mafuta katika futari zao. Badala ya kupata afya matokeo yake wanapata maradhi.
Leo nitachagua futari tatu tu, Mihogo ya nazi ama ya kuchemsha, Chapati za kusukuma ama za maji (pan cake), tambi za sukari na samaki wa kukaanga, weka na maharage ama mchuzi wa kutolea (kula na) chapati. ukipata na bhajia za kunde ama dengu ni vema kuongezea. Usisahau chai ya mkandaa (black tea) ama ya maziwa, inasaidia kuchoma matumbo (michango) na kuifanya kuwa imara.
Baada ya hapo unywe juice ya matunda ama maji ya kutosha, lakini kwa wale ambao hawana mashine za kutengenezea juice (blender), wanaweza kula matunda yenyewe, maana matunda yana nyuzi nyuzi (fiber) hivyo husaidia mmengenyo (digestion) wa chakula.
SAMAKI MCHEMSHO
Mahitaji
- Samaki 2
- Ndizi (aina yeyote, katika mapishi haya nimetumia ndizi bukoba)
- Karoti
- Pilipili hoho
- Vitunguu maji
- Chumvi
- Nyanya
- Ndimu
- Menya ndizi na uhifadhi kwenye chombo chenye maji ili zisipate kubadilika rangi
- Andaa samaki – osha, kata vipande vinavyofaa au kama unapenda mpike mzima – kamulia ndimu. Changanya samaki na limao. Kisha mhifadhi samaki pembeni.
- Andaa nyanya – osha na kisha menya nyanya 3 na kuzikata vipande vidogo. Hifadhi kwenye chombo.
- Menya vitunguu maji 2 vikubwa halafu kata kwenye vipande vidogo unavyopendelea.
- Osha na kisha kata pilipili hoho 1 kubwa kwenye vipande vidogo. Fanya vivyo hivyo kwa carrots 1 kubwa
- Weka ndizi kwenye sufuria au kikaangio kinachofaa kupikia
- Weka vitunguu maji juu ya ndizi, halafu weka nyanya juu yake, kisha malizia na karoti.
- Weka samaki wako kwenye kikaangio kwa kuwapanga vizuri juu ya karoti.
- Nyunyizia chumvi ya kutosha. Usiongeze mafuta maana kwenye samaki na vitunguu kuna mafuta ya kutosha, hivyo haina haja ya kuongeza zaidi.
- Weka maji kiasi kama kikombe 1 kikubwa halafu funika na mfuniko usioruhusu mvuke kutoka. Hii inasaidia zile mboga mboga (karoti, pilipili hoho, kitunguu na nyanya) zichuje maji yake na kukipa chakula radha na harufu nzuri.
- Subiria kwa muda wa dakika 15 hadi 20 na mchemsho wako utakuwa tayari kuliwa.
NDIZI MBIVU
VIPIMO |
Ndizi Mbivu 6
Nazi Kikopo 1
Sukari Vijiko 3 vya chakula
Hiliki Kijiko 1
NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA
1) Menya ndizi kisha zipasue kati utoe ule moyo wa kati.
2) Zikate size unayopenda mwenyewe, kisha uzipange ndani ya sufuria.
3) Weka maji kiasi na uzichemshe ndizi kidogo, karibu ya kuiva mimina tui.
4) Mimina sukari na hiliki ndani ya ndizi na ziwache zichemke mpaka tui libaki kidogo.
5) Ziondoe jikoni na uziweke kwenye sahani tayari kwa kuliwa.
KIDOKEZO:
Ni nzuri sana kuliwa na kitu cha chumvi kama nyama ya kukausha au kuku wa kuchoma.
VIAZI VYEKUNDU MASALA
Viazi Vyekundu Vya Masala
VIPIMO :
Viazi /mbatata 10 kiasi
Kitunguu maji kilichosagwa 1
Thomu iliyosagwa 1 kijiko cha supu
Pilipili iliyosagwa 1 kijiko cha chai
Rai (mustard seeds) 1 kijiko cha supu
Majani ya mchuzi (curry leaves) 7 majani
Uwatu uliosagwa (methi) 1 kijiko cha chai
Nyanya kopo 5 vijiko vya supu
Ndimu 3 vijiko vya supu
Mafuta ¼ kikombe
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
Chemsha viazi kiasi viwive lakini visivurugike
Menya, katakata vipande weka kando.
Tia mafuta katika sufuria, yakishika moto tia rai, zikaange kwa muda wa dakika moja hadi zigeuke rangi kidogo.
Tia majani ya mchuzi, uwatu, thomu, kitunguu maji, pilipili kaanga kidogo tena.
Tia nyanya kopo endelea kukaanga kidogo kisha tia chumvi, ndimu na maji kiasi kidogo ili kufanya rojo kiasi.
Mimina viazi, changanya, pakua katika sahani.
No comments:
Post a Comment