Tuesday, 7 July 2015

WATU 14 WAUAWA NA AL-SHABAAB NCHINI KENYA

Maofisa wa polisi wakiwa eneo la tukio lilipotokea shambulio lililoua watu 14 usiku wa kuamkia leo.


Takribani watu 14 wameuawa, 11 wakijeruhiwa baada ya Al-Shabaab kushambulia kijiji cha Soko Mbuzi kilichopo jirani na Mji wa Mandera, Kaskazini Mashariki mwa Kenya usiku wa kuamkia leo. Mamlaka husika huko Mandera yathibitisha.
Taswira kutoka Kijiji cha Soko Mbuzi lilipotokea shambulio.
Mashuhuda wa tukio hilo wameeleza kuwa shambulio lilitokea saa 7 usiku wa kuamkia leo wakati wakazi wa Kijiji cha Soko Mbuzi wakiwa wamelala.
Wameongeza kuwa, walianza kusikia milipuko miwili kisha ikafuatiwa na milio ya risasi. Shirika la Msalaba Mwekundu linaongoza oparesheni ya kuwaokoa majeruhi ambao idadi kamili haijulikani mpaka sasa.
Haijathibitishwa pia ni nani waliofanya shambulio hilo japo wanamgambo wa Al-Shaabab wamekuwa wakilenga wakazi wasio wenyeji wa asili katika eneo hilo walipokuwa wakitekeleza mashambulio yaliyotangulia.
Shambulio kama hilo dhidi ya wachimba migodi lilitokea jijini Mandera mwezi Desemba 2014, ambapo takriban watu 36 waliuawa na wengine wengi kujeruhiwa.
Mashambulio kama haya yametishia kudumaza shughuli katika eneo la Kaskazini-Mashariki mwa Kenya ambapo wengi wa wafanyakazi wake ni watu kutoka maeneo mingine ya Kenya.
Wafanyakazi hawa wamekuwa wakidai kutishiwa maisha. Wafanyakazi wa eneo hilo ambao wengi wao ni walimu na hata wahudumu wa afya wamesusia kurejea kazini katika eneo hilo wakidai kutishiwa maisha yao.
(Picha zote na Daily Nation)

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!