Sunday 15 March 2015

MICHEZO. NIDHAMU YAWAINGIZA VITANI MAKOCHA WA MAN CITY NA CHELSEA


Makocha wa Chelsea, Manchester City wameingia kwenye vita ya maneno kila mmoja akiwa na upande wake kuhusu nidhamu ya wachezaji nyota wa Chelsea dhidi ya waamuzi.


Msigano huo umetokana na wachezaji wa Chelsea kumzonga mwamuzi kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Jumatano dhidi ya Paris Saint- Germain (PSG).
Katika tukio la karibuni, wachezaji wa Chelsea walimzonga mwamuzi Bjorn Kuipers wakati akikaribia kutoa kadi nyekundu kwa mshambuliaji wa PSG, Zlatan Ibrahimovic kwenye Uwanja wa Stamford Bridge, jijini London. Katika tukio hilo, Ibrahimovic alitolewa nje kwa kumchezea vibaya kiungo Oscar.
Manuel Pellegrini wa Man City kwa upande wake anaamini wachezaji wa Chelsea, chini ya bosi wao, Jose Mourinho wamedekezwa kwa kiasi kikubwa, ndiyo maana wamekuwa wakiwabughudhi waamuzi wapendavyo.

Pellegrini aliliambia gazeti la The Express kuwa uamuzi huo wa nyota wa Chelsea umewafanya waamuzi wafikie uamuzi unaoipendelea klabu yao, jambo ambalo siyo sahihi katika soka.

“Siyo njia sahihi ya kusaka ushindi,” alieleza kocha huyo wakati wa maandalizi ya mechi ya Ligi Kuu England dhidi ya Burnley.
“Huwezi kuona mchezaji wangu (Man City) akimzonga mwamuzi. Pengine, unaweza kujadili uamuzi wowote na mwamuzi, hilo halitokei mara nyingi kwenye mchezo. Lakini, siamini kuwa wachezaji wa Chelsea ndivyo walivyoandaliwa ili kushinda.
“Inashangaza, kila uamuzi dhidi yao, wanamvaa mwamuzi, hilo linamzuia kufanya kazi yake apendavyo.
“Nimekuwa nikisema mara nyingi kuwa unahitaji kushinda, lakini nafikiri kuna njia tofauti za kufanya hivyo. Hata hivyo, lazima ufanye tathmini na kuamua njia sahihi ya kufanya.
“Ninazungumzia mechi kadhaa, dhidi ya timu tofauti. Lakini wamekuwa wakifanya hivyo kushinikiza mwamuzi kwa kila jambo, wanawakwaza waamuzi
MWANANCHI.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!