Sunday 15 March 2015

MAMA SALMA KIKWETE ATEMBELEA HOSPITALI YA WILAYA YA MAFIA NA SHULE YA SEKONDARI MICHENI.

1
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akikaribishwa na Mganga Mkuu wa Wilaya ya Mafia Dkt. Credianus Mgimba wakati alipokwenda kutembelea hospitali ya Wilaya, Kilindoni, kwa ajili ya kuzungumza na wafanyakazi wa hospitali na kutembelea wagonjwa tarehe 14.3.2015. Aliyesimama katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Mafia Dkt. Nassor Ali Hamid.

2


Baadhi ya wafanyakazi wa hospitali ya Wilaya ya Mafia wakifuatilia kwa makini hotuba iliyokuwa ikitolewa na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete (hayupo pichani) wakati alipotembelea hospitali hiyo tarehe 14.3.2015.
3
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na Madaktari na wafanyakazi wengine wa Hospitali ya Wilaya ya Mafia wakati alipotembelea hospitali hiyo kujionea shughuli mbalimbali za kitabibu zinazofanyika hospitalini hapo.
4
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimwangalia mtoto Naira Athuman aliyezaliwa tarehe 12.3.2015 katika hospitali ya Wilaya ya Mafia huku mama yake Fadhila Omar, mkazi wa eneo la Majengo, Kilindoni akiwa amempakata. Alisimama kushoto ni Mbunge wa Viti Maalum wa Mkoa wa Pwani Mheshimiwa Zainab Vullu.
5
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akijiandaa kumchukua mtoto mchanga Sudi Ramadhani kutoka kwa mama yake akiwa ni mtoto wa tisa kuzaliwa kwa Mama Subira Haruni, 36, mkazi wa kijiji cha Mbwela, Kata ya Mbuchi katika wilaya ya Rufiji. Wakazi wengi kutoka maeneo ya Rufiji hasa waishio katika visiwa hupendelea kwenda Mafia kupata huduma za afya ambako ni karibu kuliko Utete.
6
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na Bibi Shamsa Bwaki huku akiwa amemshika mtoto wake aliyejulikana kwa jina la Mudhihir mwenye umri wa mwezi mmoja ambaye alionekana kama amezaliwa siku moja iliyopita. Hali hiyo ilipelekea Mama Salma kupitia ushauri uliotolewa na Dkt. Hadija Mwamtemi, ambaye ni daktari wake kuamuru mtoto huyo apelekwe Muhimbili leo hii kwa ndege ili akapatiwe matibabu ya haraka.
78
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na akina mama, watoto waliokuwa maeneo ya hospitali ya Wilaya ya Mafia wakati Mama Salma alipotembelea hospitalini hapo tarehe 14.3.2015.
9
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwapungia wanafunzi, walimu na wananchi (hawapo pichani)  waliokuwa wamekusanyika katika Shule ya Sekondari Micheni iliyopo eneo la Kilindoni katika wilaya ya Mafia. Mama Salma alikwenda shuleni hapo kwa ajili ya kuzungumza na wanafunzi na walimu kuhusu mambo mbalimbali ya maendeleo ya shule hiyo.
11
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na wanafunzi, walimu na wananchi waliokusanyika katika Shule ya Sekondari ya Micheni huko Mafia. Mama Salma alikuwa kisiwani humo kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.
12
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na walimu wa Shule ya Sekondari ya Micheni mara baada ya mkutano wake na wanafunzi wa shule hiyo tarehe 14.3.2015. Aliyekaa kulia kwa Mama Salma ni Mkuu wa Shule hiyo Ndugu Seif Mohamed Gadafi. 
Picha zote na John Lukuwi

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!