Rais wa Marekani Barack Obama amelaani kile alichokitaja kuwa mauaji ya kikatili ya mmoja wa raia wa Japan aliyekuwa akishikiliwa mateka na wanamgambo wa Islamic State Haruna Yukawa.
Rais Obama pia alitaka mateka mwingine anayeshikiliwa na wanamgambo hao mwandishi wa habari Kenji Goto kuachiliwa mara moja
Kwa njia ya video Goto alionekana kwenye mitandao akishika mkononi picha ya maiti ya bwan Yukawa.
Mapema wataalamu mjini Tokyo na Marekani walisema kuwa wanatathmini ukweli wa picha hiyo.
Waziri mkuu nchini Japan Shinzo Abe alisema kuwa ameghadhabishwa na video hiyo.
No comments:
Post a Comment