Sunday, 21 September 2014

JARIDA LA WANAWAKE- UVIMBE KWENYE MFUKO WA MAYAI WA MWANAMKE (OVARIAN CYST)

KARIBU katika kona hii ya afya ili uweze kujua mengi kuhusiana na afya yako. Leo tutaangalia tatizo la uvimbe kwenye mfuko wa mayai kwa mwanamke, kwa kingereza inaitwa (ovarian cyst)


Nini maana ya uvimbe kwenye mfuko wa mayai?
Uvimbe kwenye mfuko wa mayai unatokana na mkusanyiko wa majimaji yanayozungukwa na kuta nyembamba ndani ya mayai mwanamke unajulikana kama ovarian cyst. Uvimbe huu hutokea kwa wanawake walio katika umri wa kushika mimba.
Mayai ya mwanamke ni nini?
Kwa kawaida mwanamke yoyote ana mayai mawili, yai moja upande wa kulia na yai jingine upande wa kushoto. Mayai haya upatikana pembeni ya mfuko wa uzazi (uterus), mayai haya uanza kwa kuzalishwa mayai ua uzazi ambayo ni Ovum, haya upatikana ndani ya mayai ya mwanamke (ovary) kwa kuchochewa na baadhi ya homoni.
Mayai haya ya uzazi huishi kwa masaa machache hadi masaa 24 bila kurutubishwa na mbegu za mwanaume.
Mabaki ya mfuko wa mayai ya uzazi yanayojulikana kama Follicle ndani ya ovary, hugeuka na kuwa corpus luteum ambao uhusika na utoaji wa kichocheo cha aina ya progesterone kwa wingi.
Kichocheo hichi cha progesterone ndicho husababisha mfuko wa uzazi kujiandaa kwa upachikwaji (implantation) wa yai lililorutubishwa kwa mbegu za kiume ndani ya mfuko wa uzazi kwa kuongeza unene kwenye kuta zake, yai hili usafiri hadi kwenye mfuko wa uzazi kwa ajili ya kwenda kujipachika.
Aina za uvimbe kwenye mayai ya mwanamke.
1.Follicular cyst
Aina hii unatokea baada ya vipakacha vya mayai kuzingirwa na maji lakini pale yai linaporuhusiwa kutoka kwenda katika mirija ya ya uzazi linakuwa tayari kwa ajili ya fertilization . Lakini kuna nyakati kunatokea matatizo ya homoni lile yai linakomaa na kuwa kubwa zaidi ya kawaida linashidwa kutoka kwenye vipakacha ,basi linatengeneza uvimbe na huweza kumsababishia mwanamke maumivu lakini uvimbe huu unaweza kuisha wenyewe.
2. Corpus luteum cyst
Uvimbe huu unatokea kutokana na mabaki ya tishu baada ya yai kutoka yaani katika pakacha la mayai baada ya ovum moja kupevusha vizuri huruhusiwa kutoka, corpus leteum usinyaa na kupotea wenyewe lakini inaweza kutokea corpus leteum ikajaa maji na hivyo kusababisha uvimbe wa aina hii.
Hizi ni aina mbili za uvimbe ambazo hazikai muda mrefu, unaweza ukapata uvimbe lakini ukiingia katika siku zako (menstruation) vizuri basi uvimbe huu hupotea kabisa. Mara nyingi mtu mwenye uvimbe wa aina hii matibabu yake huwa ni kupewa dawa za homoni tu ambazo zitafanya mzunguko wako kwenda vizuri.
3. Hemorrhagic cyst
Ni aina ya uvimbe ambao ndani yake kunakuwa kumejaa damu, mara nyingi hutokea wakati kukiwa na uvujaji wa damu ndani ya uvimbe wa aina yeyote ambao umeshajitengeneza tayari uambatana na maumivu makali kwenye upande mmoja wa ubavu wa mwanamke.
4. Dermoid cyst
Uvimbe huu si saratani hujulikana kama mature cystic teratoma unaathiri wanawake walio katika umri wa kushika mimba na huweza kukua na kufikia hadi inchi 6 kwa upana na ndani yake huweza kuwa na mchanganyiko wa nywele, mifupa, mafuta na cartilage.
Uvimbe wa namna hii unaweza kuwa mkubwa zaidi au kujizungusha na hivyo kuathiri usambazaji wa damu kwenda uvimbe huu na kusababisha maumivu makali.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!