Friday, 23 May 2014

CHAKULA CHA MTOTO AMBAE HAJAANZA KUTAFUNA(MCHANGA)

carrotpuree
  Mapishi ya chakula cha  mtoto ambaye bado hajaweza kutafuna vizuri. Badala ya kumpa uji na ndizi tu kuna vyakula vingi pia unaweza muandalia, hapa tutaangalia wali rojo (puree).


Mahitaji:
  • Mchele nusu kikombe kidogo
  • Karoti moja
  • Siagi
  • Maziwa fresh
Matayarisho
1. Osha mchele vizuri na kisha weka pembeni
2. Safisha karoti na katakata vipande vidogo vidogo
3. Changanya mchele, karoti na maziwa kisha ubandike jikoni, na chumvi kidogo sana ili kuleta ladha
4. Vikianza kuchemka weka siagi kiasi na acha hadi kiive kabisa, hakikisha kinakuwa rojo rojo
5. Epua na kisha saga kny mashine au kwa kutumia mwiko.
6. Chakula tayari kwa kumpa mtoto. Unaweza weka na mchicha kidogo au njegere ila angalia usichanganye vitu vingi sana anaweza akakinai.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!