TIMU ya watoto wa mitaani ya Tanzania kutoka Kituo cha Mwanza, inaendelea vizuri katika mashindano ya Kombe la Dunia kwa watoto hao yanayoendelea Rio de Janeiro nchini Brazil, ambako mchezo wake wa kwanza ilikwenda sare ya mabao 2-2 na Burundi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura, Machi 31 mwaka huu, timu hiyo inayoongozwa na mjumbe wa mkutano mkuu wa shirikisho hilo kutoka Mkoa wa Mwanza, John Kadutu, ilicheza mechi mbili. Katika mechi ya kwanza iliifunga Argentina mabao 3-0 na baadaye ikailaza Nicaragua 2-0.
Michuano hiyo ya siku kumi inashirikisha timu kumi. Mbali ya Tanzania, nyingine ni Argentina, Burundi, India, Kenya, Liberia, Marekani, Mauritius, Misri na Pakistan. Kwa wasichana ni Afrika Kusini, Brazil, El Salvador, Indonesia, Msumbiji, Nicaragua, Philippines, Uingereza na Zimbabwe
No comments:
Post a Comment