Sunday 7 July 2013

PENNY NA SAUDA MWILIMA, WAKIJUMUIKA KATIKA NDOA YA SHOSTY WAO DIDA AMBAYE SASA NI RASMI DIDA WA EZDEN"


 VJ Penny, Ezden, Deen, Dida na Sauda Mwilima...

TBS YAPIGA MARUFUKU UUZWAJI WA MAFUTA YA KUPIKIA, AINA YA OKI, SI SALAMA YANA MADHARA KWA AFYA








Shirika la Viwango Tanzania (TBS), limebaini kuwa mafuta ya kula aina ya Oki na Viking yaliyoenea sokoni nchini, yamebainika kuwa hayafai kwa matumizi ya binadamu.
Kwa mujibu wa TBS, vipimo vyote vitatu vilivyotumika kuyapima kuonyesha ubora, vimefeli na vimeonyesha mafuta hayo kuharibika kwa haraka tangu yalipotengenezwa na mpaka leo.

TAMASHA LA MATUMAINI LAFANA, WENGI WAJITOKEZA KUSHUHUDIA

...Akiwakagua…
Rais Kikwete akielekea kukagua timu.
Rais Kikwete akisaini mpira utakaotumika.
...Akiwakagua Yanga.picha zote na GPL









JANUARY MAKAMBA AWATAKA WANANCHI WAWALAUMU WABUNGE WAO KUHUSU KODI YA 1000 KWA KILA LAINI.....ADAI WIZARA YAKE ILIPINGA VIKALI






Haya  ni  majibu ya  Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mh. January Makamba akijibu maswali katika mtandao wa Twitter kuhusu kodi mpya ya TZS 1000 kwa mwezi kwa kila line ya simu. 

  •  Amesema kwamba Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia iliipinga kodi hiyo. Amesema kwamba Hazina (Wizara ya Fedha) walikubaliana na
  •  maoni ya Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia kuhusu kodi hiyoAmesema kwamba Bunge ndilo lililopitisha kodi hiyo na si Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia.

  • .

BASI LA SUMRY LATUMBUKIA MTONI NA KUUA TISA, NA KUJERUHI 53 HUKO KATAVI.


Na Willy Sumia, Katavi
KATIKA hali isiyo ya kawaida basi la kampuni ya Sumry limetumbukia mtoni na kuuwa watu tisa na kujeruhi abiria wapatao hamsini na tatu katika mto Iku uliopo katika kijiji cha Sitalike wilaya ya Mlele mkoani Katavi.

Tukio hilo la kusikitisha lilitokea saa sita usiku kuamkia Julai 5, 2013 basi hilo lilipokuwa likitokea mjini Sumbawanga kuelekea Mpanda mkoani Katavi likiwa na abiri waliokuwa wametoka Mbeya.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Katavi Emanuely Nnley alisema jana kuwa ajali hiyo ilihusisha basi aina ya Nissan Diesel lenye namba T909 AZT mali ya kampuni ya Sumry lililokuwa likiendesha na dereva aliyetajwa kwa jina na Stephano Chimane maarufu kwa jina la Ntungu.

Alisema basi hilo lilipofika katika daraja hilo lenye kona kali na mteremko dereva wake alishindwa kulimudu na kulenga daraja hali iliyosababisha tairi za nyuma kupanda juu ya ukingo na kudumbukia mtoni ambapo dereva wa basi hilo aliweza kutoka na kukimbilia kusikojulikana.

Alifafanua kuwa juhudi za uokoaji zilianza kufanyika usiku huo huo ambapo majeruhi 53 waliokolewa na maiti tisa za wanaume watatu na wanawake watano na motto mmoja wa kike ziliopolewa katika maji.

Alisema hali ya majeruhi inaendelea vizuri isipokuwa majeruhi watatu walikimbizwa katika hospitali ya mkoa wa Rukwa kwa matibabu zaidi na kufafanua kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva kushindwa kuliongoza gari, ubovu wa gari na wembamba wa daraja
Akizungumza na gazeti hili Afisa Mwandamizi wa SUMATRA mikoa ya Rukwa na Katavi, David Chiragi alisema basi hilo lilikuwa limeiba njia kwani leseni yake inaliruhusu basi hilo kufanya safari za Sumbawanga Kirando na siyo Sumbawanga Mpanda kwa mujibu wa leseni iliyotolewa mwezi Juni mwaka huu.


NDEGE YA KENYA AIRWAYS IMELAZIMIKA KUTUA UGIRIKI KWA AJILI YA KUONEKANA ISHARA YA NDEGE HIYO KUWAKA MOTO.



Mtandao wa Standard Digital unaripoti kuwa ndege yenye namba KQ117  iliyokuwa na jumla ya abiria  ilitua salama katika uwanja wa Athens kisha abiria wote na wafanyakazi wa ndege kupelekwa hotelini kwaajili ya kupisha uchunguzi wa chanzo cha ishara ya tahadhari ya moto katika eneo la mizigo la ndege hiyo.

Taarifa hiyo imeendelea kusema uchunguzi katika kifaa cha kugundua dalili za moto ulifanyika ili kubaini chanzo, lakini hakuna tatizo lolote lililoonekana.

Baada ya ukaguzi huo abiria walikuwa wanategemewa kuondoka Athens kuendelea na safari ya Nairobi majira ya saa 11 jioni ya leo.


YASEMEKANA HAWA NDIO WANAWAKE WAWILI WAZURI KULIKO WOTE DUNIANI, TUMA MAONI YAKO JE NI KWELI?




photo

photo

photo

photophotophoto



photo

 

Fathima Kulsum Zohar Godabari who was once a royal Princess is now an official Queen in Saudi Arabia.

She was recently photographed without niqab covering her face and the pictures were published on the internet, exposing her beautiful facial features to the world for the first time.
Since the release of the pictures, many have argued her to be the most beautiful woman on earth

BANGI NAVUTA, UNGA HELL NO" MSIKIE TID AKIMTOLEA UVIVU SPORA SHOW, UJEURI WA UHAKIKA MPAKA MWISHO WA INTERVIEW......

ICHEKI HAPA EXCLUSIVE INTERVIEW YA 
MSANII T.I.D TOKA TANZANIA ALIYOFANYIWA 
NCHINI UINGEREZA KWENYE KIPINDI CHA 
SPORAH SHOW NA MWANADADA SPORAH NJAU

WEMA SEPETU REALITY SHOW COMING SOON!



Saturday 6 July 2013

WEEKEND NJEMA WADAU WA SOPHIE MBEYU BLOG, KANYAGA TWENDE NA DIAMOOONDOO! NAWAPENDA AISEE!!!


MTANZANIA ALIYEKUWA MASOMONI AUAWA NA VIBAKA MAREKANI.


sykes_omar-2
Omar Sykes wa Howard University DC enzi za uhai wake
POLISI wametambua mwili wa mwanafunzi wa Howard University aliyeuawa kwenye jaribio la uhalifu Alhamisi usiku.
Omar Sykes, 22, na mwanafunzi mwenzake walikuwa wanatembea maeneo ya 700 block of Fairmont Street NW kabla ya saa 5.30 usiku walipofuatwa na watu wawili. 

Polisi wanaamini kulikuwa na jaribio la uhalifu ila yalitokea mabishano kabla mmoja ya wale watu kutoa bastola na kumuua Sykes. Alifikia mauti kwenye hospitali ya maeneo ya jirani.
“Tunadhani ilikuwa jambo la ghafla na hatuna uhakika kama wanafunzi hao waliibiwa mali yoyote” alisema Kapteni Bob Alder wa kituo cha polisi DC alipohojiwa na News4.
Mwanafunzi mwingine alipigwa na kitako cha bastola na kujeruhiwa kichwani ingawa hana majeraha makubwa. 

“Wanafunzi wengi wamepatwa na hofu ya kutoka na kutembea usiku kwani hali hii inaogopesha sana,” alisema mwanafunzi mmoja alipohojiwa na Megan McGrath kutoka News4.
Maelezo kamili kuhusu watuhumiwa bado hayajapatikana. Kulikuwa na matukio mengi ya kujumuisha watu wakati wa tukio hivyo polisi wanatumaini kuwa haitawia vigumu kwa wahalifu hao kujulikana.
Sykes alipenda uandishi na mara ya mwisho aliandika makala kwenye mtandao unaoitwa Our Black Pages mnamo tarehe 11 Juni. Wasifa wake unaonesha kwamba alikuwa anasomea Marketing na Public Relations. Mkesha wa sala kwa ajili ya marehemu utafanyika shuleni kwao Jumamosi kuanzia saa 1 usiku.
Howard University imetoa maelezo yafuatayo kuhusiana na kifo cha Alhamisi:
“Tuna huzuni kubwa kufuatia kifo cha mmoja wa wanafunzi wetu kilichotokea nje ya shule. Mwanafunzi mwingine alijeruhiwa kwenye tukio hilo na anaendelea na matibabu…. Polisi wa Howard University wanashirikiana polisi wa mji ili kupeleleza tukio hili hatari. Tunawapa pole familia, shule na wale wote walioguswa na tukio hili kwa namna moja au nyingine. Huduma ya ushauri nasaha itapatikana masaa 24 kwa wanafunzi wote watakaohitaji msaada katika kipindi hiki kigumu.” 
 
Chanzo. Sunday shomari blog.

WAZAZI WAUA MTOTO WAKIGOMBANIA CD YA MSANII "DIAMOND"



Vilio  na  simanzi  vilitanda Jumatano iliyopita Mwananyamala Kisiwani, jijini Dar kufuatia mtoto wa mwaka mmoja, Rahim Rajab kufariki dunia kwa kuangukiwa na watu watatu, akiwemo baba yake mzazi, Rajab Said..


Tukio la watu hao kumwangukia mtoto huyo lilitokea Jumatatu iliyopita na lilisababishwa na ugomvi mkubwa wa CD yenye nyimbo za mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ ulioibuka ndani ya chumba cha kulala kati ya mama wa marehemu na mpangaji mwenzake aitwaye Aisha.


Akizungumza kwa machungu kuelezea tukio hilo, mama mzazi wa marehemu Rahim, Habiba Ally alikiri kuwa kisa cha kifo cha mwanaye ni CD tu.Akasema:
 
CHANZO MPEKUZI.

MASANJA MKANDAMIZAJI KUHUBIRI NENO LA MUNGU MAREKANI


Mtumishi wa Mungu Emmanuel Mgaya (Masanja Mkandamizaji) ambaye yuko nchini Marekani kwa ziara maalum, atahudumu kwa waumini wa jiji la Washington DC na vitongoji vyake siku ya kesho (Jumapili 07/07/2013) 
 
Bwana  Mgaya ambaye pia hufahamika kama Mchungaji Mtarajiwa  na ambaye amekuwa akifanya huduma ya uhubiri nchini Tanzania, atahubiri katika ibada ya jumapili katika kanisa la THE WAY OF THE CROSS GOSPEL MINISTRIES katika ibada ya kawaida ya kila jumapili ambayo hufanyika kuanzia saa saba kamili mchana mpaka saa tisa kamili alasiri (1:00pm - 3:00pm)

Hii itakuwa ni huduma ya kwanza nchini Marekani kwa Mtumishi huyu ambaye ni Mchungaji msaidizi katika kanisa la EAGT Mito ya Baraka lililopo Kariakoo jimbo la Temeke jijini Dar Es Salaam likiongozwa na Askofu Bruno Mwakibolwa na ameshafanya huduma katika sehemu mbalimbali nchini Tanzania.

VUNJA MBAVU!

HUYU NAE NIAJE?

RAHA JIPE MWENYEWE! CHEZEYAA ! HATA SIJUI NI WIMBO GANI ANACHEZA .......

Mpe a.k.a huyu rafiki yangu!

RICHARD BEZUIDENHOUT APEWA TUZO YA KUWA MSANII BORA WA FILAM.

 Richard Bezuidenhout starred as a lead actor in the movie Zamora that just received an Award at the Khouribga African Film Festival in Morocco. This is the first time an East African film garners this prestigious award. Richard was also the winner of BIG BROTHER AFRICA in 2007



This is not LB APPAREL news but its a good news to me because one of my brothers, Richard Bezuidenhout starred as a lead actor in the movie Zamora that just received an Award at the Khouribga African Film Festival in Morocco. This is the first time an East African film garners this prestigious award. Richard was also the winner of  BIG BROTHER AFRICA in 2007. 

http://www.screenafrica.com/page/news/africa/1631206-Zamora-triumphs-at-Khouribga
Shams Bhanji (centre) with lead actors -
Richard Bezuidenhout and Richa Adhia







 

MALKIA WA MIPASHO KHADIJA KOPA AELEZEA KUHUSU KIFO CHA MUMEWE.




Malkia wa Mipasho Bongo, Khadija Kopa.

BAADA ya mumewe kipenzi, Jafar Ally kufariki dunia hivi karibuni, Malkia wa Mipasho Bongo, Khadija Kopa amefunguka kuwa kwa sasa anaishi maisha magumu sana.

Marehemu Jafar Ally enzi za uhai wake.

Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni, mwanamama huyo alisema hali hiyo inatokana na kukosa msaada aliokuwa akiupata kutoka kwa mumewe huyo ambaye alikuwa na nafasi kubwa katika maisha yake.
“Hakika naishi maisha magumu sana hivi sasa, sina hata nguvu ya kufanya chochote ila namshukuru Mungu kwa yote, mume wangu alikuwa ndiyo msaada mkubwa kwangu, nikienda kwenye shoo ananipeleka sasa nimebaki mpweke, siwezi kumsahau mume wangu milele,” alisema Khadija.
Kwa upande mwingine, Khadija alisema hana mpango wa kuolewa tena kwa sasa kutokana na jinsi alivyokuwa akimpenda mumewe japokuwa hawezi kujua kwa siku zijazo kwani Mungu ndiye mpangaji wa kila jambo.

JITIBU MAGONJWA 27 KWA ASALI NA MDALASINI


Mdalasini 
Asali  
                       MDALASINI NA ASALI

Taswira  ya  mtu  anayesumbuliwa  na  tatizo  la  chunusi  ambalo  linaweza  kuondoka  kwa  kutumia  mdalasini  kama  makala  haya  yanavyo  elekeza. 
" MDALASINI NA ASALI vinaweza kukufanya uonekane kama picha yenye afya nzuri.
Asali inafahamika vema Duniani kote kama mojawapo ya silaha ya kiajabu katika kupigana na
magonjwa na matatizo yatokanayo na uzee.
Sasa hivi, utafiti mpya umeonyesha kwamba uwezo wa asali unaweza kuongezwa maradufu kama
itachanganywa na mdalasini wa kawaida.
Uchunguzi wa kina ufanywao kwa wiki na jarida la World News wa Tiba, wataalamu wa madawa
yatokanayo na mimea pamoja na kijarida cha afya na lishe, imeonekana kwamba kuna dazani nyingi za
umuhimu wa asali na mdalasini pamoja na michanganyiko {dawa} ya kusisimua iletayo afya bora.
Kama ifuatayo
 
  1. UGONJWA WA VIUNGO MAUMIVU NA UVIMBE(ARTHRITIS),
  2.   Wataalamu wa lishe wanapendekeza kuchukua kwa kutumia mchanganyiko wa sehemu moja ya asali
    pamoja na sehemu mbli za maji vuguvugu na kijiko kimoja {cha chai} chenye mdalasini - na kuchua
    sehemu zilizoathirika. Nafuu hupatikana katika muda wa dakika moja.
    Vinginevyo tengeneza chai-kikombe kimoja chenye maji moto, weka vijiko vya chakula -viwili vya
    asali kwa kijiko cha chai cha mdalasini. Kunywa asubuhi na jioni ili kuondoa maumivu
KUKATIKA KWA NYWELE.
 
 Asali ikishachanganywa na mdalasini pamoja na mafuta vuguvugu ya olive, hutoa kichocheo
maridhawa cha kuotesha nywele kinachotumika katika dawa ya Dork. Mchanganyiko huo vuguvugu
unapakwa kwa kusugua kichwani na kuachwa kwa dakika 15
 
 
 
UKUNGU  WA MIGUU (FUNGUS)
 
Wataalamu wa lishe wanapendekeza kuchukua kwa kutumia mchanganyiko wa sehemu moja ya asali
pamoja na sehemu mbli za maji vuguvugu na kijiko kimoja {cha chai} chenye mdalasini - na kuchua
sehemu zilizoathirika. Nafuu hupatikana katika muda wa dakika moja.
Vinginevyo tengeneza chai-kikombe kimoja chenye maji moto, weka vijiko vya chakula -viwili vya
asali kwa kijiko cha chai cha mdalasini. Kunywa asubuhi na jioni ili kuondoa maumivu.
 
ENDELEA KUWA NASI WIKI IJAYO KWA MUENDELEZO WA MATUMIZI NA FAIDA ZA MDALASINI NA ASALI................
 
 

DIDA MTIKISIKO ATIKISA NA NDOA, HAPA BAADA YA KUFUNGA NDOA NA MUMEWE EZDEM



Kila la kheri BI DADA!

MPAKA MIAKA YA LEO BADO KUNA BAADHI YA SHULE HAZINA MADAWATI, SHULE HII MOJAWAPO KATIKA MKOA WA MBEYA

          

MWALIMU WA SHULE YA MSINGI YA UHURU ILIYOPO TUNDUMA WILAYA YA MOMBA MKOANI MBEYA ADELA MTWEVE AKIONESHA NAMNA AMBAVYO WANAFUNZI WA DARASA LA PILI KATIKA SHULE YA MSINGI UHURU WANAVYOKETI WANAPOKUWA DARASANI

MWANDISHI WA HABARI WA STAR TV AMINA SAIDI AKIJARIBU KUKETI KATIKA TOFARI KUJARIBU KUANDIKA KAMA AMBAVYO WANAFUNZI WA DARASA LA PILI WA SHULE YA MSINGI UHURU WANAVYOANDIKA


KILIO CHA SHULE HIYO KIMEANZA KUSIKILIZWA NA WADAU ZIKIWEMO TAASISI MBALIMBALI ZA KIFEDDHA AMBAPO BENKI YA POSTA TANZANIA ILIJITOLEA MIFUKO 100 KWA AJILI YA KUSAIDIA UJENZI WA SHULE HIYO

Friday 5 July 2013

MITINDO YA VITENGE


Mitindo ya Vitenge inaweza kushonwa katika dizain mbalimbali, hii inaonyesha mitindo kwa vijana ni katika kuonyesha kuwa kitenge si lazima liwe gauni unaweza kumshonea binti yako pia akapendeza

yes!

Afrocentric Ankara.
Watoto pia hawajasahaulika, wanapendeza na vitenge.....

CuteIt's African-inspired.


 maxi dress <3 African Prints in Fashion: Prints of the Week: Taibo Bacar

.
JAMANI HATA KHANGA INAWEZA KUPENDEZA IKISHONWA VIZURI, HII NI MITINDO YA KHANGA..

MASANJA NA SHILOLE WAKITALII NCHINI MAREKANI, WATEMBELEA VOA NA WHITE HOUSE.

Kutoka kushoto ni Mery Mgawe, Hadija Riyam, Shilole, Sunday Shomari, Dr. Hamza Mwamoyo, Ilham Dirran, Masanja na Raymond Maro katika picha ya pamoja wakati wasanii Shilole n Masanja walipotembelea studio za Voice Of America Idhaa ya Kiswahili Jijini Washington.
Msanii Shilole akifanyiwa mahojiano ya Luninga na mtangazaji wa VOA, Sunday Shomari
Msanii Masanja Mkandamizaji akifanyiwa mahojiano ya Luninga na mtangazaji Sunday Shomari.
Wasanii Shilole na Masanja wakifanyiwa mahojiano ya Radio na mtangazaji wa VOA idhaa ya Kiswahili, Sunday Shomari.
Wasanii Masanja na Shilole wakipata picha nje ya mjengo wa Voice Of America.
Msanii Masanja akipata picha nje ya jengo jeupe (white House), Ikulu ya ya Rais wa Marekani
Msanii Shilole akipata picha nje ya jengo jeupe alipokwenda yeye na Masanja kutembele mjengo huo.
Shilole na Masanja wakiwa nje ya jengo jeupe
Shilole na Masanja katika picha ya pamoja na Mdau Liberatus Mwang'ombe kulia ni watoto waliokua wakipata nao picha za kumbukumbu kutoka kwa wazazi wao (hawapo pichani)
Masanja akiwa katikati ya mktaa wa Pennsylvania, mtaa ulipo jengo jeupe.
Wasanii Masnja na Shilole wakikatiza kitaa cha Pennsylvania
 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!