Sunday 7 July 2013

NDEGE YA KENYA AIRWAYS IMELAZIMIKA KUTUA UGIRIKI KWA AJILI YA KUONEKANA ISHARA YA NDEGE HIYO KUWAKA MOTO.



Mtandao wa Standard Digital unaripoti kuwa ndege yenye namba KQ117  iliyokuwa na jumla ya abiria  ilitua salama katika uwanja wa Athens kisha abiria wote na wafanyakazi wa ndege kupelekwa hotelini kwaajili ya kupisha uchunguzi wa chanzo cha ishara ya tahadhari ya moto katika eneo la mizigo la ndege hiyo.

Taarifa hiyo imeendelea kusema uchunguzi katika kifaa cha kugundua dalili za moto ulifanyika ili kubaini chanzo, lakini hakuna tatizo lolote lililoonekana.

Baada ya ukaguzi huo abiria walikuwa wanategemewa kuondoka Athens kuendelea na safari ya Nairobi majira ya saa 11 jioni ya leo.


No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!