Saturday 6 July 2013

MALKIA WA MIPASHO KHADIJA KOPA AELEZEA KUHUSU KIFO CHA MUMEWE.




Malkia wa Mipasho Bongo, Khadija Kopa.

BAADA ya mumewe kipenzi, Jafar Ally kufariki dunia hivi karibuni, Malkia wa Mipasho Bongo, Khadija Kopa amefunguka kuwa kwa sasa anaishi maisha magumu sana.

Marehemu Jafar Ally enzi za uhai wake.

Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni, mwanamama huyo alisema hali hiyo inatokana na kukosa msaada aliokuwa akiupata kutoka kwa mumewe huyo ambaye alikuwa na nafasi kubwa katika maisha yake.
“Hakika naishi maisha magumu sana hivi sasa, sina hata nguvu ya kufanya chochote ila namshukuru Mungu kwa yote, mume wangu alikuwa ndiyo msaada mkubwa kwangu, nikienda kwenye shoo ananipeleka sasa nimebaki mpweke, siwezi kumsahau mume wangu milele,” alisema Khadija.
Kwa upande mwingine, Khadija alisema hana mpango wa kuolewa tena kwa sasa kutokana na jinsi alivyokuwa akimpenda mumewe japokuwa hawezi kujua kwa siku zijazo kwani Mungu ndiye mpangaji wa kila jambo.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!