“Tunawaahidi mashabiki kwamba tutafanya shoo ya saa mbili mfululizo, wakati tunafanya shoo hii ni wakati mwafaka kwa wasanii wa Tanzania kujifunza kutoka kwetu nini tunafanya tukiwa jukwaani ili kuzidi kujenga wanamuziki wakubwa kutoka Afrika. Tunahitaji Waafrika tutambulike kimataifa kama ilivyo kwa P Square na hii ni kaulimbiu yetu,” alisema Peter.Kundi la PSquare linaundwa na ndugu wawili pacha Peter na Paul Okoye ambao walisema wasanii wa Tanzania wana nafasi kubwa ya kujifunza kutoka kwao kupitia tamasha hilo ambalo ni mara ya pili kufanya nchini Tanzania tangu mwaka 2008 walipofanya tamasha lililojulikana kama ‘Do Me Concert’.
Naye Paul alivitaka vyombo vya habari kupigania haki za wasanii na kuwatangaza kwani Tanzania ina vijana wanaojituma katika kazi za sanaa.
“Huu ni wakati wa sisi wasanii kubadilishana mawazo P Square tunaweza kufanya kazi na wasanii wa Tanzania ili kuinua muziki wao pia, lakini vyombo vya habari vina nafasi kubwa ya kuwainua wasanii.”
Chanzo: Mtanzania
No comments:
Post a Comment