Saturday, 23 November 2013

MTOTO SELEMAN RAJABU AENDA KUTIBIWA INDIA, AWASHUKURU WALIOGUSWA NA KUMCHANGIA


Mtoto Seleman Rajabu (16) ambaye mguu wake ulianza kuvimba wenyewe tangu alipozaliwa.
Stori: Imelda Mtema
MTOTO Seleman Rajabu (16) ambaye mguu wake ulianza kuvimba wenyewe tangu alipozaliwa, amechangiwa fedha zaidi ya Sh. Mil. 4 ambazo zimemwezesha kwenda nchini India kupata matibabu.
Akizungumza na mwandishi wetu, kijana huyo alisema hana chochote cha kuwalipa Watanzania waliojitolea kumsaidia, bali atawaombea kwa Mungu ili awabariki kwani maumivu ya mguu wake yanampa mateso makubwa.
“Nawashukuru sana wote walionichangia kwa moyo wao wa huruma na kuona ni jinsi gani ninateseka kila siku, nitazidi kuwaombea kwa Mungu wazidi kufanikiwa zaidi,” alisema Sele.
GPL

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!