
Wanawake wawili wa tanzania, wamekamatwa katika uwanja wa ndege wa Tambo J,burg Afrika ya kusini, wakisafirisha madawa ya kulevya aina ya Methamphetamine, yenye ujazo wa kilo 150. Habari zinasema Kiasi hicho kikubwa zaidi hakijawahi kukamatwa katika mpaka wowote wa nchi hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyoripotiwa na shirika la habari la Africa Kusini SABC siku ya Ijumaa (July 5), msemaji wa South African Revenue Services (SARS) Marika Muller amesema, wanawake hao waliowasili na ndege kutoka Tanzania, walikutwa na mabegi 6 makubwa yaliyojaa madawa (crystal meth) yenye thamani ya Rand 42.6 million ambayo ni sawa na zaidi ya billion 6 ya Tanzania.
Wakati huohuo, taarifa zinasema Watanzania wengine wawili wamekamatwa na madawa ya kulevya katika uwanja wa Julius Kambarage Nyerere, wakiwa na Madawa yenye thamani ya shilingi Mil 90.
VIDEO YA HABARI KUHUSIANA NA WANAWAKE HAO WALIOKAMTWA













No comments:
Post a Comment