
Rais Jakaya Kikwete amewataka wananchi kuwa makini na wanasiasa wanaotumia kila njia kuweka reheni amani na utulivu uliopo nchini kwa kuwa hawana nia njema na tunu adhimu ya amani iliyoipa Tanzania sifa kubwa duniani.
Rais Jakaya Kikwete amesema baadhi ya viongozi wa dini na vyama vya siasa wamekuwa wakifanya mambo ambayo yamekuwa yakiweka rehani hali ya utulivu na amani iliyopo hapa nchini hivyo kutaadharisha wananchi kuwa makini na watu hao kwa kuwa hanawa nia njema na tunu yetu nadhimu ya amani iliyotupa sifa kubwa duniani.
Rais Kikwete amesema hayo wakati akifunga kongamano la kitaifa la kujadili amani ya taifa lililoandaliwa na kituo cha taifa cha demokrasia Tanzania - TCD na kuongeza kuwa kamwe serikali haitavumilia watu wa namna hiyo ambao wamelenga kuhakikisha amani ya nchi inakuwa hatarini.
Katika mkutano huo rais Kikwete amesema wananchi wanapaswa kutambua kuwa vurugu za aina yoyote zitakazo tokea nchini zitakuwa na athari kubwa kwa taifa hivyo ni bora wanaotaka kufanya hivyo kutengwa na jamii.
Kwa upande wake mwenyekiti wa tcd Mh James Mbatia amesema vyama vya siasa vimekubaliana kulinda amani kwa gharama yoyote ili tanzania izidi kuwa mahali pazuri kwa watu na mali zao.
Naye muasisi wa tcd Mh John cheyo amesema vyama vya siasa vinatakiwa kuwa muongozo katika kuimarisha amani na umoja wa kitaifa.Kongamano hilo lilishirikisha wadau mbalimbaliwa maswala ya amani pamoja na siasa hapa nchini













No comments:
Post a Comment