Jeshi
la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia watu wanane, akiwamo
mfanyakazi wa ndani anayetuhumiwa kumuua mfanyakazi mwenzake kwa
kumchinja.
Kamanda
wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, alisema hayo
alipozungumza na waandishi wa habari jana.
Alisema
Philemon Laiza (27), mkazi wa Mikocheni B, anatuhumiwa kuhusika na mauaji ya
Perptua Maina (30) kwa kumchinja na kisha kutelekeza mwili wake kwenye dampo la
takataka.
Alisema baada ya polisi kufanya upelelezi mtuhumiwa alikutwa na kiatu kimoja cha
marehemu na nguo alizovaa siku ya tukio, ambazo zilikuwa zimetapakaa
damu.
Kamishna Kova alisema kuwa mtuhumiwa alipohojiwa alidai kuwa
marehemu alitoweka nyumbani tangu siku ya Ijumaa na baada ya kubanwa na polisi
mtuhumiwa alikiri kuhusika na tukio hilo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)














No comments:
Post a Comment