Joseph Mbilinyi ‘Sugu’.
USHUHUDA WA SUGU
Ukweli wa jinsi matajiri wauza
unga wanavyowatumia wanamuziki wa Kitanzania kama punda, unapewa nguvu na
ushuhuda aliowahi kuutoa Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi
‘Sugu’.
Mbunge huyo ambaye anapewa
heshima kwamba ni mmoja wa waasisi wa Bongo Fleva, alimweleza mwandishi wetu
kuwa kabla hajawa memba wa jumba hilo la kutunga sheria, aliwahi kufuatwa na
wauza unga kumshawishi awe anabeba mzigo kwenda nao nje ya nchi.
Mwaka 2011, mbunge huyo aliwahi
kugusia hilo, wakati akitoa hoja kuchangia bajeti ya Wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo kuwa serikali ni lazima iwasaidie wanamuziki wa Kitanzania
kwa sababu wanaibiwa sana, hivyo kuwafanya vijana kuona kimbilio rahisi la
kutajirika ni kuuza madawa ya kulevya.
“Mheshimiwa spika, serikali
isifanye ili kijana wa Kitanzania afanikiwe lazima auze unga, madawa ya
kulevya,” alisema Sugu na kueleza mfano huo wa jinsi alivyofuatwa kushawishiwa
na matajiri wa unga ili naye awe punda.Source. Fahari ya Mwananchi.













No comments:
Post a Comment