Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na
Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mke wa Rais wa Mali Madam
Traore Mintou Doucoure wakati wa hafla ya ukaribisho iliyofanyika huko New York
tarehe 11.6.2013.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na
Mwanzilishi na Rais wa Shirika la Voice of African Mother’s Inc.la nchini
Marekani Mrs Nana-Fosue Randal wakati wa tafrija ya kuwakaribisha wake wa Marais
kutoka barani Afrika watakaotunukiwa tuzo ya Millenium Development Goals
itakayotolewa tarehe 13.6,2013.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa pamoja na
wake wa Marais wa Afrika wakati wa tafrija ya kuwakaribisha iliyofanyika katika
ukumbi wa UN Milenium Hotel tarehe 11.6.2013. Wengine katika picha ni Mke wa
Rais wa Mali Madam Traore Mintou Doucoure, Mke wa Rais wa Equatorial Guinea
Madam Constancia Mangue Nsue de Obiang na wa mwisho ni Mwanzilishi na Rais wa
Shirika la Voice of African Mother’s Inc la nchini Marekani Mrs Nana-Fosue
Randal.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiingia kwenye tafrija
akiongozana na Mke wa Rais wa Equatorial Guinea Madam Constancia Mangue Nsue de
Obiang













No comments:
Post a Comment