Friday, 14 June 2013

NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI ZAWASILISHA BAJETI ZAKE.

Waziri-wa-Fedha-Tanzania
Mawaziri wa fedha wa mataifa manne ya afrika mashariki, kenya, Uganda, Tanzania na Rwanda wamesoma bajeti ya nchi zao kwa mwaka 2013 -2014.
Kwa sehemu kubwa nchi zote zinaongeza matumizi kwa ajili ya maendeleo ya nishati na miundo mbinu. Hata hivyo Uganda imepandisha bei ya mafuta na bidhaa muhimu jambo ambalo litaweza kuzusha malalamiko mapya nchini humo.
Serikali ya Kenya imetangaza bajeti yake chini ya mfumo mpya ya utawala na serikali ndogo zaidi. Mwandishi wetu wa Nairobi Mwai Gikonyo anasema hii ni mara ya kwanza kwa waziri wa fedha kusoma bajeti ambayo inazingatia zaidi maslahi ya wananchi walio wengi.
Kwa upande wa Tanzania mwandishi wa VOA Dina Chahali anasema bajeti imezingatia maeneo sita muhimu ya maendeleo ya nchi.
Bajeti ya Uganda inazingatia zaidi kuimarisha mipango ya nishati, miundo mbinu na mawasiliano ameeleza leylah Ndinda mwandishi wa VOA Kampala.
Na Rwanda serikali inajisifu kwa kufanikiwa kupunguza kutegemea msaada kutoka kwa wahisani kukamilisha mahitaji ya matumizi yake kwa mwaka na maendeleo ya nchi.

SURCE VOICE OF AMERRICA(VOA)

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!