MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini
Tanzania Mwana FA anafikiria kuahirisha shoo yake ya kesho kufuatia kifo cha
msanii mwenzake wa kizazi kipya Langa Kileo, kilichotokea leo jijini Dar es
Salaam.
Mwana FA anafikiria kuahirisha shoo yake
ya kesho iliyopangwa kufanyika katika viwanja vya Makumbusho ya Taifa jijini Dar
es Salaam na tayari ameanza kuwasiliana na meneja wake kwa ajili ya hatua
hiyo.
Hii itakuwa ni mara ya pili kwa Mwana FA
kuahirisha shoo yake, awali ilipaswa kufanyika Mei 31 mwaka huu lakini
ikaahirishwa kutokana na kifo cha aliyekuwa msanii mwenzake wa Bongo Fleva
Albert Mangwea.
Hata hivyo Mwana FA ametoa tahadhara ya
kejeri juu ya hatua hiyo huku akimtupia madongo mhasimu wake mkubwa Mwanadada
Lady Jay Dee...
Katika taarifa yake aliyoitupia katika
mtandao wa kijamii wa Facebook Mwana FA amesema kwamba:
7 minutes ago via mobile · Like
Mwana FA Halisi : "Msiba wa mwana HIPHOP mwenzetu Langa unanifanya nifikirie
kuahirisha show ya kesho. Nawasiliana na manager wangu kisha nitawajuza ,but si
kwa kumuogopa mwanamke,Let it be clear"
7 minutes ago via mobile · Like
Mwana FA Halisi : "Msiba wa mwana HIPHOP mwenzetu Langa unanifanya nifikirie
kuahirisha show ya kesho. Nawasiliana na manager wangu kisha nitawajuza ,but si
kwa kumuogopa mwanamke,Let it be clear" 














No comments:
Post a Comment