
Mtoto wa MJ Paris Jackson ameripotiwa kwenye vyombo vya habari vya Marekani kuwa alitaka kujiua baada ya kukata kiganja chake cha mkono wake na kunywa vidonge Jumatano, baada ya hapo mtoto huyo mwenye umri wa miaka 15 alitoa taarifa na kukimbizwa hospitali.
Alifikishwa katika hospitali ile ile aliyofariki baba yake Michael Jackson na anaendelea na matibabu chinzi ya uangalizi maalum wa madaktari wa akili.
Lakini ni nini hasa chamsumbua Paris? wachambuzi wanaeleza mtoto huyo hakutaka kujiua ila tu alitaka kufikisha ujumbe kwa walezi wake, siku chche kabla ya tukio hilo alitoa ujumbe wa aina mbali mbali kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter na siku za nyuma katika mahojiano yake na Oprah Winfrey ameeleza kilio chake cha kudai kupewa uhuru wa kuwa na maisha ya kawaida kwani anataka akue kama watoto wenzake shuleni na sio kulindwa wakati wote.
Aliongeza katika ujumbe wake anapenda sana kutumia muda wake mwingi na mama yake mzazi Debbie Rowe kwani huko anakuwa katika maisha ya kawaida na si kulindwa kila wakati. Sikiliza ripoti ya ENTV hapa.













No comments:
Post a Comment