Thursday, 6 June 2013

KILIMANJARO MUSIC AWARD KUWA HEWANI KWENYE MITANDAO YOTE



Usiku wa tuzo za Muziki Tanzania maarufu kama Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2013 unatarajiwa kuonyeshwa live mtandaoni siku ya Jumamosi, Juni 8.

Tofauti na miaka mingine ambayo tukio la utoaji tuzo tu ndio lilikuwa likionyeshwa kupitia kwenye TV pekee, na kuwanyima fursa Watanzania waishio nje ya nchi kufuatilia moja kwa moja, mwaka huu watumiaji wa mtandao wa Internet wataweza kuangalia toka mwanzo tukio la Red Carpet litakaloanza saa moja jioni wakati wanamuziki na watu wengine mashuhuri wakiwasili ukumbini.
Pia tukio la utoaji tuzo litakaloanza rasmi saa tatu usiku litakuwa moja kwa moja mtandaoni hadi litakapofikia mwisho. 


Watumiaji wa simu za Android, Blackberry, iPhone na tablets wanaweza ku-download application ya *LIVESTREAM* itakayowawezesha kuangalia moja kwa moja kwenye simu zao wakati watumiaji wa computer watatazama kupitia http://new.livestream.com/KTMA2013/live na katika Blogs mbalimbali



 




 

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!