
MREMBO aliyejulikana kwa jina la Pepetua Maina au maarufu kama Lucy, Mkikuyu wa Kenya anayekadiriwa kuwa na miaka 25 mpaka 30 amekutwa amekufa kwa kuchinjwa shingo na mwili wake kutupwa katika shimo la taka
Mwili wa huo ulikutwa na polisi Juni 8, mwaka huu Mikocheni B, jirani kabisa na makazi ya Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova.
Kwa mujibu wa mtoa habari, mwili wa msichana huyo uligunduliwa na msichana mmoja mfanyakazi wa ndani, alipoenda kutupa taka katika sehemu hiyo, na kwamba alipiga kelele za mshituko, ndipo majirani walipotoka na kujionea wenyewe.
Taarifa za polisi zimesema kuwa msichana huyo kabla ya kuchinjwa alipigwa vibaya kwani mkono wake mmoja wa kushoto ulikuwa umevunjwa, na kwamba alikutwa na jeraha moja kubwa kwenye paji la uso, na pia marehemu alikuwa amechnjwa shingoni, na kiganja cha kushoto kilikatwa na kitu chenye ncha kali.
Kutokana na maelezo ya majirani walisema hawakuwahi kusikia kelele zozote usiku huo, na kwamba huenda msichana huyo aliuliwa sehemu nyingine na kuja kutupwa katika eneo hilo.
Imefahamika kwamba msichana huyo(marehemu) alikuwa mfanyakazi wa jaji aliyetambulika kwa jina la jaji Kileo.
Mwili wa msichana huyo umehifadhiwa katika hospitali ya M/nyamala, na kwamba mtu mmoja anashikiliwa na polisi kuhusiana na tukio hilo













No comments:
Post a Comment