
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Mkoani Tabora Mhashamu Paulo Luzoka ameitahadharisha Tume ya mabadiliko ya katiba na jamii kwa ujumla juu ya rasimu ya katiba iliyotolewa hivi karibuni, kuhusiana na serikali tatu, kuwa iwe makini na mambo ambayo yanaweza kuleta kuvunjwa muungano na kuleta mgawanyiko.
Askofu Luzoka amesema haoni sababu ya kuwepo na serikali tatu ikizingatiwa kuwepo kwa changamoto za uendeshaji, huku akidai kuwa, kwa namna moja ama nyingine, maadui wanaweza kutumia udhaifu wa kiongozi mmojawapo na kusababisha mgawanyiko, na machafuko.













No comments:
Post a Comment