Tuesday 13 July 2021

Wagonjwa 408

 

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Dr. Dorothy Gwajima amesema Watu 408 wamebainika kuwa na ugonjwa wa covid 19 unaosababishwa na virusi vya corona nchini Tanzania huku 284 wakiwa katika mashine za oksijeni.


Itakumbukwa juzi July 07,2021, Rais Samia Suluhu akiwa Kibaigwa alisema ———> “Nimetazama hapa (Kibaigwa) ninaowaona Watu walioziba midomo na pua ni kidogo sana, nataka niwaambie tuchukue tahadhari zote dhidi ya maradhi ya Corona, wimbi la tatu lipo kwenye Nchi na hakuna la kuficha, tayari tuna wagonjwa kwenye Mikoa ya DSM, Arusha, Mwanza na mingine hata Dodoma kwa kiasi kidogo sana lakini wapo”

“Chukueni tahadhari hili wimbi la tatu ambalo linapukutisha wenzetu lisije kupukutisha hapa kwetu, gonjwa hili likianza kutuangusha halina kusimama linapukutisha tu”

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!