Saturday 17 July 2021

TATIZO LA UMEME WA MOYO "ATRIAL FIBRILLATION" MAANA YAKE NINI?

 



Tatizo la umeme wa Moyo ni pale ambapo Chemba za juu za moyo zinazohusika na kusukuma damu kwenye moyo (Atria) zinashindwa kufanya kazi sawa sawa kupelekea kushindwa kushirikiana na chemba ziingine za chini (Ventricles) kuisukuma damu kuingia na kutoka kwenye moyo kwenda sehemu ziingine za mwili.

Umeme wenyewe wa moyo ni pale ambako moyo wenyewe unazalisha nguvu(umeme) itakayosaidia hivi vyumba vyake kusukuma damu. Umeme huu huzalishwa na kundi la seli hai ziitwa sinus node ambazo hupatika katika Chemba ya juu kulia(Right atrium).
DALILI ZA TATIZO LA UMEME WA MOYO
Mtu anapopata tatizo hili mapigo yake ya moyo huenda kasi sana kufikia mapigo100 hadi 175 kwa dakika,Maumivu ya kifua sehemu ya kulia, kuishiwa pumzi na kuchoka mwili mzima.
NINI VISABABISHI VYA TATIZO
Visababishi vya tatizo hili viko vingi vikiwemo mtu kuzaliwa na matatizo ya moyo kutofanya kazi vizuri, Shinikizo la damu, kama mtu alishawahi kufanyiwa upasuaji wa moyo, moyo kupata maambukizi, Umri kua mkubwa moyo kufifia uwezo wake wa kufanya kazi nk.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!