Tuesday 2 June 2020

George Floyd: Je ni kipi kilichotokea dakika 30 za mwisho kabla ya kifo chake?

George Floyd
Haki miliki ya pichaTWITTER/RUTH RICHARDSON
Image captionGeorge Floyd mara kwa mara aliwaambia maafisa waliomkamata kwamba hawei kupumua
Marekani imekabiliwa na maandamano ya kitaifa kuhusu kifo cha M'marekani mweusi aliyekua amekamatwa na maafisa wa polisi.

George Floyd , 46 alifariki baada ya kukamtwa na maafisa wa polisi nje ya duka moja katika mji wa Minneapolis katika jimbo la Minnesota.

Kanda ya video ya tarehe 25 mwezi Mei inamuonyesha afisa wa polisi mzungu , Derek Chauvin , akiwa amepiga magoti katika shingo ya bwana Floyd huku akiwa amezuiliwa chini katikati ya barabara.


    Bwana Chauvin ,44 kwa sasa ameshtakiwa kwa mauaji.

    Matukio yaliopelekea kifo cha bwana Floyd yalitokeo katika kipindi cha dakika 30 .
    Kulingana na walioshuhudia , kanda ya video na taarifa rasmi, hiki ndicho tunachokijua.
    Ilianza na ripoti kuhusu noti bandia ya $20. Ripoti ilitolewa jioni ya tarehe 25 Mei, wakati bwana Floyd alinunua pakiti ya sigara katika duka la Cup foods.
    Baada ya kuamini kwamba noti ya dola 20 aliyoitoa Floyd ilikuwa bandia , mfanyakazi mmoja wa duka hilo aliripoti kwa polisi.
    Bwana Floyd alikuwa akiishi katika mji wa Minneapolis kwa miaka kadhaa baada ya kuhama kutoka Houston katika jimbo la Texas.
    Alikuwa akifanya kazi kama mlinzi mjini humo, kama mamilioni ya raia wengine wa Marekani, alikuwa amepoteza kazi yake kutokana na mlipuko wa virusi vya corona.
    Bwana Floyd alikuwa mteja katika dula la Cup Foods .
    ''Alikuwa rafiki wa duka hilo, mteja mzuri ambaye hakusababisha tatizo lolote'' , mmiliki wa duka hilo Mike Abumayyaleh aliambia chombo cha habari cha NBC.
    Lakini bwana Abumayyaleh hakuweko kazini siku ya tukio hilo. Katika kuripoti kuhusu noti hiyo bandia, mfanyakazi wake kijana alikua anafuata itifaki za kazi.
    Baada ya kupiga simu ya 911 mwendo 20.01, mfanyakazi huyo alimtaka Floyd kurudisha sigara hizo , lakini Floyd alikataa kurudisha kulingana na maandishi yaliotolewa na mamlaka.
    Mfanyakazi huyo alisema kwamba Floyd alionekana kana kwamba amekunywa pombe na hakuweza kujizuia , yalisema maandishi hayo. Muda mfupi baada ya simu mwendo wa 20.08, Maafisa wawili wa polisi waliwasili.
    Bwana Floyd alikuwa ameketi na watu wengine wawili katika gari ambalo lilikuwa limeegeshwa katika kona moja.
    Baada ya kulikaribia gari hilo, afisa mmoja wa polisi, Thomas Lane , alitoa bunduki yake na kumuagiza bwana Floyd kuonyesha mikono yake.
    Wakizungumza kuhusu tukio hilo, waendesha mashtaka hawakuelezea kwa nini bwana Lane aliamua kutoa bunduki yake.
    Bwana Lane, waendesha mashtaka walisema walishika mikono ya Floyd na kumvuta nje ya gari hilo. Baadaye bwana Folyd akakataa kufungwa pingu.
    Baada ya kufungwa pingu, bwana Floyd alikubali kushikwa huku bwana Lane akielezea alikuwa anakamatwa kwa kutoa pesa bandia.
    Ni wakati maafisa wa polisi walipojaribu kumuingiza wbana Floyd katika gari lao ndiposa mvutano ukatokea.
    Mwendo wa 20.14, bwana Floyd alikataa na kuanguka chini na kuwaambia maafisa wa polisi kwamba ana tatizo la 'uoga ama hofu', kulingana na ripoti hiyo.
    Bwana Chauvin aliwasili katika eneo hilo. Yeye na maafisa wengine walihusika katika jaribio jingine kumuingiza bwana Floyd ndani ya gari.
    Wakati wa jaribio hilo ,20.19, bwana Chauvin alimvuta bwana Floyd nje kutoka katika kiti cha abiria na kumuangusha chini , ripoti hiyo ilisema.
    Alilala hapo uso wake ukiwa chini bado akiwa amefungwa pingu.
    Ni wakati huo ambapo mashahidi walianza kumrekodi bwana Floyd, ambaye alionekana kuwa katika hali ngumu.
    Tukio hilo ambalo lilirekodiwa katika simu nyingi na kusambazwa sana katika mitandao ya kijamii lilikua la mwisho la bwana Floyd.
    Bwana Floyd alizuiliwa na maafisa , huku bwana Chauvin akimwekea goti lake katikati ya kichwa chake na shingo.
    'Siwezi kupumua', bwana Floyd alisema na kurejelea mara kwa mara , akimlilia mamake na kuomba tafadhali, tafadhali ,tafadhali.
    Kwa dakika 8 na sekunde 46, bwana Chauvin aliweka goti lake katika shingo ya Bwana Floyd , ilisema ripoti ya mwendesha mashtaka.
    Derek Chauvin, 44, anatarajiwa kuwasilishwa mbele ya mahakama ya Minneapolisi siku ya JumatatuHaki miliki ya pichaREUTERS
    Image captionDerek Chauvin anatarajiwa kufika mbele ya mahakama katika mji wa Minneapolis siku ya Jumatatu
    Dakika sita baada ya tukio hilo, bwana Floyd alikuwa amepoteza fahamu .
    Katika kanda ya video ya tukio hilo , bwana Floyd alinyamaza huku mashuhuda wakimtaka afisa huyo wa polisi kuchunguza mishipa yake ya damu iwapo bado alikuwa hai.
    Mmoja wa maafisa hao JA Kueng, alifanya hivyo , akiutazama mkono wa kulia wa bwana Floyd, lakini hakuweza kupata mshipa hata mmoja.
    Lakini maafisa hao hawakumuachilia. Mwendo wa 20.27 , bwana Chauvin aliondoa goti lake kutoka shingo ya bwana Floyd .
    Akiwa amepoteza fahamu , bwana Floyd alipelekwa katika kituo cha afya cha Hennepin akiwa ndani ya ambyulansi.
    Alitangazwa kuwa amefariki saa moja baadaye.
    Usiku kabla ya kifo chake , bwana Floyd alizungumza na rafikiye mmoja wa karibu , Christopher Harris .
    Alikuwa amemshauri bwana Floyd kuzungumza na mawakala wa kazi za muda.
    ''Kughushi , alisema , sio tabia ya bwana Floyd. 'Jinsi alivyofariki ni ukatili mkubwa' , alisema Harris.
    Aliomba uhai wake. aliomba uhai wake. Unapojaribu kuweka imani kwa mfumo huu, mfumo ambao unajua hakutengenezewa wewe , unapotaka haki mara kwa mara na hauwezi kupata unaanza kuchukua sheria mikononi mwako.
    BBC.

    No comments:

     

    ADVERTISE WITH US

    AFRICAN FASHION

    PLACE YOUR ADS HERE!