Friday 31 January 2020

CORONA: Watanzania wanaosoma China waliopo nchini watakiwa kutorudi Vyuoni

Serikali imewataka Wanafunzi wanaosoma China ambao wako likizo nchini Tanzania, kutorudi nchini humo kwanza hadi pale zitakapopatikana taarifa za Kidiplomasia kuhusiana na ugonjwa unaosababishwa na Virusi vya Corona.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema hayo Bungeni na kueleza kuwa Wizara ya Mambo ya Nje inaendelea kufanya mawasiliano na Balozi zote mbili juu ya mwenendo wa ugonjwa huo.
Amesema, Serikali itakaporidhika na hali inayoendelea nchini China itatoa tamko kwa Watanzania walioko likizo kurudi kuendelea na masomo na iwapo hali ikiendelea kuwa mbaya sana itatafuta utaratibu mwingine.
CRD: MillardAyo.com

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!