Thursday, 12 January 2017

Daktari Asogeza Mbele Kesi Ya ‘Scorpion’

scorpioni-1


scorpioni-2
Salum Njwete ‘Scorpion’ akiingia Mahakama ya Mwanzo Ilala, Dar.
scorpioni-4
Mwandishi wa Global Publishers na mtandao huu, Issa Mnally (kulia mwenye kamera) akiwa mahakamani hapo.
scorpioni-5
Scorpion akiongea jambo na askari Magereza.

scorpioni-6
Wananchi wakiwa eneo la mahakama

scorpioni-7
Kesi ya kujeruhi na unyang’anyi wa kutumia silaha inayomkabili Salum Njwete ‘Scorpion’, leo imeshindwa kuendelea baada ya daktari aliyemtibu majeruhi anayetajwa katika kesi hiyo, Said Mrisho kushindwa kutokea mahakamani.
Katika viunga vya Mahakama ya Wilaya ya Ilala, kama kawaida umati uliokuwa ukitaka kusikiliza kesi hiyo ulifurika mapema asubuhi kutaka kujua kinachoendelea.
Ilipofika mishale ya saa mbili na nusu, Scorpion alifikishwa mahakamani hapo akitokea Gereza la Ukonga na kuhifadhiwa kwa muda kwenye mahabusu ya mahakama hiyo.
Saa tatu kamili chumba cha mahakama kilikuwa tayari kimeandaliwa kwa ajili ya kesi hiyo ambapo Wakili wa Scorpion, Juma Nasoro, Wakili Mwandamizi wa Serikali, Nasoro Katuga, Hakimu anayeendesha kesi hiyo, Frola Haule na makarani wote walikuwa tayari kwenye chumba inapoendeshwa kesi hiyo wakimsubiri mtuhumiwa huyo apelekwe ili kesi iendelee.
Saa tatu na robo maafande wa magereza zaidi ya nane wengine wakiwa na silaha nzito walimchomoa Scorpion na kumpeleka kwenye chumba cha mashitaka mbele ya hakimu, Frola Haule.
Scorpion akiwa kizimbani, Wakili Katuga aliiambia mahakama hiyo kuwa kesi hiyo ilifika mahakamani hapo kwa ajili ya shahidi wa nne upande wa Jamhuri ambaye ni daktari aliyemtibu majeruhi kutoa ushahidi wake.
Wakili huyo alisema shahidi huyo alitoa udhuru mahakani hapo kuwa asingeweza kufika mahakamani hapo kwa kuwa yuko nje ya kituo cha kazi hivyo ameomba kesi hiyo iahirishwe na shahidi huyo apewe wiki mbili au tatu.
Baada ya ombi la wakili huyo, mahakama hiyo iliahirisha kesi hiyo mpaka Januari 25 mwaka huu ambapo Scorpion alirudishwa rumande.
Kwa hisani ya GPL.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!