KOMAMANGA ni tunda lenye asili ya India na Persia, kwa jina la kisayansi linaitwa Punica Granatum. Lakini lililetwa Marekani na wawekezaji wa Kihispania na kwa sasa limejulikana dunia nzima. Komamanga si tunda tu, bali ni chakula chenye vitamini, madini pamoja na virutubisho vingine vingi vinavyoweza kufanya miili yetu kuwa na afya na nguvu tele. Virutubisho vinavyopatikana katika komamanga ni vitamin C kwa wingi, vitamin B5, vitamin A, vitamin E, Madini ya Potassium na Iron.
Juisi ya mbegu za komamanga husaidia kuponya saratani, pia husaidia mtiririko wa damu kwenda vizuri katika mishipa ya damu, hivyo kupunguza hatari ya magonjwa ya moyo, shinikizo la damu na kiharusi.
Huzuia meno kuoza na kuhuisha mfumo wa kinga mwilini kwa kuondoa vijidudu, bakteria na maambukizi ya virusi ndani ya mwili.
Pia husaidia kutibu maradhi ya tumbo ikiwamo kutopata choo. Komamanga hutumika kama tunda, kutengeneza juisi, pia hutumika likiwa limepikwa.
Mti wake una faida nyingi mno katika mwili wa mwanadamu.
Mti wake una faida nyingi mno katika mwili wa mwanadamu.
Una virutubisho vingi vinavyopatikana kwenye magome, majani, mbegu, maganda ya matunda, juisi ya matunda pamoja na kwenye maua ya mti wake.
Zifuatazo ni faida muhimu za mti wa mkomamanga:
1. Maganda ya tunda la mkomamanga yakichemshwa hutoa juisi ambayo hutumika kama dawa ya kufunga kuhara.
2. Majani ya mkomamanga hutumika kutibu hali ya tumbo kujaa gesi na kudhibiti tindikali (acid) tumboni.
3. Majani ya mkomangana hutumika pia katika kutibu tatizo la kuhara damu maambukizi ya bakteria katika kibofu cha mkojo.
4. Rojo ya mbegu za mkomamanga ikichanganywa na maziwa ya ng’ombe, hutumika kutibu tatizo la mawe kwenye figo.
5. Fukuto ya komamanga husaidia kutibu minyoo aina ya tegu pamoja na uvimbe wa wengu.
6. Komamanga husaidia katika kutibu tatizo la vidonda vya tumbo.
7. Komamanga pia ni mahiri katika kutibu magonjwa ya kusendeka (magonjwa ya muda mrefu), kama vile saratani ya tezi dume, saratani mbalimbali, kisukari, baridi yabisi na uvimbe katika maungio ya vidole (gout)
8. Komamanga husaidia kuondoa sumu mwilini.
9. Husaidia katika kupambana na tatizo la uzito mwilini.
10. Husaidia kuua virusi vya aina mbalimbali mwilini.
No comments:
Post a Comment